Korea Kusini
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: 널리 인간을 이롭게 하라 "Lete faida kwa watu wote" | |||||
Wimbo wa taifa: Aegukga (Wimbo la Taifa) | |||||
Mji mkuu | Seoul | ||||
Mji mkubwa nchini | Seoul | ||||
Lugha rasmi | Kikorea | ||||
Serikali | Jamhuri Moon Jae-in (문재인 , 文在寅) Kim Boo-kyum (김부겸 , 金富謙) | ||||
Kuundwa kwa Ufalme wa Gojoseon Tangazo la uhuru bado chini ya Japani Ukombozi kutoka utawala wa Japani Jamhuri ya kwanza ilitambuliwa na Umoja wa Mataifa |
3 Oktoba 2333 KKa 1 Machi 1919 15 Agosti 1945 15 Agosti1948 12 Desemba 1948 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
100,210 km² (ya 108) 0.3 | ||||
Idadi ya watu - Julay 2014 kadirio - Msongamano wa watu |
50,617,045 (ya 26) 505.1/km² (ya 13) | ||||
Fedha | Won ya Korea Kusini (KRW )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
Wakati sanifu wa Korea (UTC+9) -- (UTC+9) | ||||
Intaneti TLD | .kr | ||||
Kodi ya simu | +82
- |
Korea ya Kusini (jina rasmi: Jamhuri ya Korea) ni nchi ya Asia ya Mashariki iliyopo kusini mwa rasi ya Korea.
Upande wa kaskazini imepakana na Korea ya Kaskazini. Korea zote mbili zilikuwa nchi moja hadi mwaka 1945 chini ya utawala wa kikoloni wa Japani.
Ng'ambo ya bahari iko Uchina upande wa magharibi na Japani upande wa kusini-mashariki.
Mji mkuu, pia mji mkubwa, ni Seoul ambako karibu nusu ya wakazi wote huishi ama mjini ama katika mazingira yake. Seoul ni kati ya miji muhimu ya biashara na uchumi kimataifa.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Utamaduni wa Korea ni kati ya zile za kale zaidi duniani.
Tangu maungano ya kitaifa ya Korea yote mwaka 668 KK ilikuwa nchi moja hadi mwaka 1910 ilipofanywa koloni la Japani.
Uhuru baada ya mwaka 1945 ulifuatwa na mgawanyiko wa nchi na kuundwa kwa Korea Kusini.
Awali ilikuwa nchi maskini yenye uchumi wa kilimo, lakini iliendelea kuwa nchi ya viwanda iliyofaulu kusogea mbele na kujenga demokrasia imara.
Siku hizi imekuwa moja ya nchi tajiri ya Asiaː ina nafasi ya 13 duniani kati ya mataifa matajiri. Iko kati ya nchi kumi duniani zinazouza bidhaa nyingi nje.
Hali ya maisha ni ya juu na viwanda vyake vinatengeneza bidhaa za kisasa kabisa kama motokaa, meli, mashine, vifaa vya kompyuta na nyinginezo.
Miji
[hariri | hariri chanzo]Mikoa
[hariri | hariri chanzo]Kuna mikoa tisa nchini Korea Kusini, zikiwemo:
- Chungcheongbuk-do
- Chungcheongnam-do
- Gangwon-do
- Gyeonggi-do
- Gyeongsangbuk-do
- Gyeongsangnam-do
- Jeju-do
- Jeollabuk-do
- Jeollanam-do
Watu
[hariri | hariri chanzo]Wakazi karibu wote (99 %) ni Wakorea asili. Wachina ni 1.8 %, lakini wengi wao wana asili ya Korea.
Idadi ya watu inaelekea kupungua kutokana na uzazi kuwa wa nadra mno (watoto 9 kwa watu 1,000ǃ).
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kikorea.
Dini
[hariri | hariri chanzo]Kiasili watu wa Korea walifuata dini ya jadi iliyoheshimu mapepo mbalimbali na kutoa sadaka kama njia za kuyapatanisha.
Tangu karne ya 4 Ubuddha uliingia kutoka China ukawa dini rasmi.
Ukonfusio ulifuata tangu karne ya 13.
Ukristo ulingia pia kutoka China ukaanza kukua zaidi tangu karne ya 19.
Siku hizi takriban nusu ya Wakorea wa kusini wasema hawana dini. Sehemu kubwa wanakadiriwa kuwa wafuasi wa Konfusio lakini hawajiiti "wanadini".
Ukristo ni kundi kubwa la kidini ukiwa na 29 % za Wakorea wa Kusini, wakiwemo Waprotestanti (18.3 %) na Wakatoliki (10.9 %). Wabuddha ni kama 22.8 %. Kuna pia wafuasi wachache wa dini nyingine mbalimbali.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiingereza) Korea.net: Gateway to Korea portal from the KOIS government agency; tovuti rasmi
- Discover Korea and its cuisine Ilihifadhiwa 24 Julai 2010 kwenye Wayback Machine.
- Information about Working and Living in South Korea Ilihifadhiwa 3 Julai 2007 kwenye Wayback Machine.
- South Korean Military Pictures Ilihifadhiwa 27 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine. DefenceTalk
- BBC News - Country Profile: South Korea
- Encyclopaedia Britannica, South Korea - Country Page
- CIA World Factbook - South Korea Ilihifadhiwa 3 Julai 2015 kwenye Wayback Machine.
- Guardian Unlimited - Special Report: North and South Korea
- Korea National Statistical Office
- Korea Peace Network Ilihifadhiwa 9 Desemba 2006 kwenye Wayback Machine. summary of past/current American policy towards Korea
- Library of Congress - Country Study: South Korea data as of Juni 1990
- National Assembly official site
- Open Directory Project - South Korea Ilihifadhiwa 18 Desemba 2006 kwenye Wayback Machine. directory category
- Tour2Korea operated by Korea National Tourism Organization
- South Korea travel guide kutoka Wikisafiri
- Yahoo! - South Korea Ilihifadhiwa 17 Desemba 2006 kwenye Wayback Machine. directory category
- Yahoo! News - Full Coverage: South Korea
- Galbijim Wiki for expats in Korea
- South Korea main cities satellite views and latitude and longitude coordinates Ilihifadhiwa 4 Februari 2010 kwenye Wayback Machine.
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |