Gojoseon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gojoseon

Gojoseon (고조선, 古朝鮮) ulikuwa ufalme wa kale wa Korea. Ufalme huu hehasabiwa kama taifa sahihi kabisa la watu wa Korea. Kwa mujibu wa Samguk Yusa na rekodi nyingine za zama za kati za Kikorea,[1] Gojoseon inasemekana kwamba ilianzishwa mnamo 2333 KK na mkongwe Dangun, ambaye anasemekana kwamba anatokea kwenye Ukoo wa Mbinguni (天孫, 천손). Ilikuwa katikati ya beseni la Mto Liao na upande wa kaskazini mwa Peninsula ya Korea.

Watu wa Gojoseon[hariri | hariri chanzo]

Watu wa Gojoseon waliishi huko kaskazini-mashariki mwa Manchuria ya kale na hutazamiwa kama ndugu wa kwanza kunadikwa kwenye rekodi za Korea.[2] Watu wa Gojoseon walikuwa wakirekodiwa kwenye maandiko kadhaa ya Kichina wakiwa kama moja kati ya Dongyi, maana yake "washenzi wa mashariki".

Watu wa Gojoseon walikuwa vizazi vya kabila la wahamiaji wa Altaic waliolewea huko Manchuria, mashariki ya mbali ya Uchina, na Peninsula ya Korea. Gojoseon hatimaye wakajikita kwenye eneo dogo la Manchuria na Peninsula ya Korea.

Eneo[hariri | hariri chanzo]

Awali, Gojoseon huenda ilikuwa mjini Liaoning; lakini kunako 400 KK, ikahamia karibu na Pyongyang, mji mkuu wa sasa wa Korea Kaskazini.[3][4]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tazama pia Jewang Ungi, Dongguk Tonggam, Sejong Sillok, na Chronicle of Korean Rulers, Jewang yeondaeryeok (제왕연대력, 帝王年代曆), imeandikwa na Choe Chiwon (최치원) (857 – ?)
  2. Jaehoon Lee (2004). "The Relatedness Between The Origin of Japanese and Korean Ethnicity". The Florida State University. uk. 31. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-14. Iliwekwa mnamo 2007-04-11. 
  3. "고조선[古朝鮮". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-30. Iliwekwa mnamo 2009-10-30. 
  4. "Timeline of Art and History, Korea, 1000 BC – 1 AD". Metropolitan Museum of Art. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-07. Iliwekwa mnamo 2009-10-30. 
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gojoseon kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.