Peninsula ya Korea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Peninsula ya Korea
Location of the Korean peninsula
Map of the Korean peninsula

Peninsula ya Korea ni peninsula iliopo Asia ya Mashariki. Imepanuka kuelekea upande wa kusini kwa takriban maili 684 (1,100 km) kutoka barani Asia hadi katika Bahari ya Pasifiki na imezungukwa na Bahari ya Japani (pia inaitwa Bahari ya Mashariki) kwa upande mashariki, Bahari ya Uchina ya Mashariki upande wa kusini, na Bahari ya Manjano upande wa magharibi, kwenye Mlango wa Korea unaounganisha njia mbili za kwanza za maji.

Hadi mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Korea ilikuwa sehemu moja ya kisiasa ambayo kwa haraka-haraka ilipata kugonga hadi kwenye eneo la Peninsula ya Korea. Tangu kusimamishwa kwa Vita ya Korea mnamo 1953, nusu ya sehemu ya kaskazini ilikuwa imechukuliwa na Korea Kaskazini, wakati nusu ya kusini ilichukuliwa na Korea Kusini.

Mipaka ya kaskazini ya Peninsula ya Korea inaeleweka kikawaida kwamba imepakana baina ya Korea Kaskazini na majirani zake wa kaskazini, Uchina (1,416 km ikiwa pamoja na mikoa ya Jilin na Liaoning) na Urusi (19 km). Mipaka hii imejiumba kiasili na mito ya Yalu/Amnok na Tumen/Tuman/Duman. Kwa kuchukua ufafanuzi huu, Peninsula ya Korea (ikiwa pamoja na visiwa vyake) ina eneo la kilomtia za mraba zipatazo 220,847 (85,270 sq mi).

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Peninsula ya Korea kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.