Pyongyang

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Pyongyang
Nchi Korea Kaskazini
Metro ya Pyongyang.
Jiji gizani.
Mnara wa Juche.

Pyongyang (kwa Kikorea: 평양 직할시 'Phyŏngyang chighalshi' kwa mwandiko wa Kilatini) ni mji mkuu, pia mji mkubwa wa Korea Kaskazini wenye wakazi 2,926,443 na pamoja na rundiko la mji watu 3,702,757 (2005). Ni kati ya mahali pachache ambako wageni wa nje wanaruhusiwa kutembelea.

Mji uko kusini-magharibi mwa nchi, karibu na mpaka na Korea ya Kusini. Pyongyang ni kitovu cha nchi kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Pyongyang ni mji wa kale kwenye rasi ya Korea. Kuna hakika ya kwamba kituo cha biashara ya Kichina kiliundwa karibu na mji uliokuwepo tayari.

Mwaka 427 ilitajwa mara ya kwanza kama mji mkuu wa ufalme.

Mji ulivamiwa na Wajapani kuanzia mwaka 1592 hadi 1593 halafu na China mwaka 1627.

Katika karne ya 19 wamisionari wengi walifika Pyonyang wakajenga zaidi ya makanisa 100. Idadi ya Wakristo iliongezeka hadi kufikia theluthi moja ya wakazi wote kabla ya Ukomunisti kuchukua serikali lakini baadaye imepungua kama dini zote.

Mji uliharibiwa vibaya katika vita vya Japani dhidi ya China ya 1894–1895. Chini ya utawala wa Japani kati ya 1910 hadi 1945 viwanda vingi vilijengwa.

Vita vya Korea ya 1950–1953 ilileta tena uharibifu mwingi. Baadaye mji ulijengwa upya kwa muundo wa miji ya Umoja wa Kisovyeti pamoja na bustani kubwa na barabara pana.

Hali ya maisha[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwisho wa Ukomunisti katika Urusi na mabadiliko katika China uchumi wa Korea Kaskazini umeporomoka. Zaidi ya nusu ya viwanda vya Pyongyang vimefungwa. Umeme unapatikana kwa masaa pekee.

Watazamaji hukadiria ya kwamba njaa mjini si kali kama vijijini na kwenye miji mingine kwa sababu mji mkuu hupendelewa katika mgawanyo wa vyakula na bidhaa chache zinazopatikana.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pyongyang kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.