Bagamoyo (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Wilaya ya Bagamoyo

Lua error in Module:Location_map at line 510: Unable to find the specified location map definition: "Module:Location map/data/Tanzania" does not exist.Mahali pa Bagamoyo katika Tanzania

Majiranukta: 6°26′24″S 38°53′24″E / 6.44000°S 38.89000°E / -6.44000; 38.89000
Nchi Tanzania
Mkoa Pwani
Wilaya Bagamoyo
Bagamoyo katika miaka ya 1890.

Bagamoyo ni mji mwambaoni mwa Bahari Hindi katika Tanzania takriban km 75 kaskazini kwa Dar es Salaam na km 45 magharibi kwa kisiwa cha Unguja.

Vyanzo vidogo[hariri | hariri chanzo]

Bagamoyo iko kati ya miji ya kale kabisa ya Waswahili katika Tanzania. Magofu ya Kaole (msikiti na makaburi ya karne ya 13 BK) yako karibu na Bagamoyo yakionyesha umuhimu wa utamaduni wa Kiislamu katika eneo hili. Lakini hakuna uhakika kuhusu historia ya Bagamoyo ya kale isipokuwa ya kwamba mnamo karne ya 18 mji haukuwa muhimu. Wakazi walio wengi wakati ule walikuwa wavuwi na wakulima, palikuwa na biashara kiasi cha samaki na chumvi.

Mlango wa misafara ya Afrika ya Kati[hariri | hariri chanzo]

Mwisho wa karne ile familia za Waarabu kutoka Oman walihamia Bagamoyo wakipanua biashara yake. Mji ukawa kituo muhimu zaidi kwenye pwani; biashara ya misafara mikubwa ya karne ya 19 kwenda barani hadi Kongo ilianza na kurudi hapa.

Bandari ya watumwa[hariri | hariri chanzo]

Hasa kuhamia kwa makao ya Sultani wa Oman kuja Zanzibar kuliongeza umuhimu wa mwambao karibu na Unguja. Wafanyabiashara wa Zanzibar walikusanya bidhaa zao huko Unguja wakavuka bahari na kuajiri mahamali. Wakarudi miezi au miaka kadhaa baadaye wakileta pembe za ndovu na watumwa. Kwa njia hiyo Bagamoyo ilijulikana kama bandari kuu ya biashara ya watumwa kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki katika karne ya 19. Watumwa wakasafirishwa kwa jahazi au dhau hadi Unguja wakiuzwa huko sokoni.

Kanisa Katoliki Bagamoyo

Mapadre wa Roho Mtakatifu walijenga kituo chao cha kwanza katika Afrika ya Mashariki huko Bagamoyo wakiona umuhimu wa mji kama mlango wa bara.

Mji mkuu wa koloni la Kijerumani[hariri | hariri chanzo]

Aprili 1888 Sultani wa Zanzibar alikodisha eneo la pwani kwa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki walioanzisha makao makuu yao Bagamoyo. Ukali wa kampuni ulisababisha katika muda wa wiki chache ghasia ya wenyeji wa pwani iliyoleta vita vya Abushiri ambavyo vilikandamizwa na wanajeshi wa Ujerumani. Mwaka 1890 serikali ya Ujerumani ilichukua madaraka ya utawala badala ya kampuni halafu mji mkuu ukahamishwa Dar es Salaam.

Umuhimu wa Bagamoyo ilianza kupungua tena kwa sababu meli kubwa zilitumia bandari ya Dar es Salaam badala ya Bagamoyo.

Mji wa kisasa[hariri | hariri chanzo]

Leo hii Bagamoyo ni mji mdogo unaofanywa na kata mbili za Magomeni na Dunda. Majengo yake ya kihistoria yako katika hali mbaya. Wakazi walio wengi wanaishi katika sehemu jipya la Magomeni na soko jipya. Majaribio ya hifadhi la urithi wa kihistoria hayakufaulu sana tangu miaka mingi.

Mzee katika mji mkongwe wa Bagamoyo

Bagamoyo ina chuo cha kitaifa kiitwacho Chuo cha Sanaa cha Bagamoyo. Kinafundisha uchoraji wa jadi wa Tanzania, uchongaji, mchezo, kucheza na kucheza. Mwaka 2007 kulingana na chuo, Sanaa ya Bagamoyo na Taasisi ya Kitamaduni (TaSuba) ilianzishwa. Mzee katika mji mkongwe Bagamoyo Tangu 2002 barabara ya lami imepatikana na kuleta matumaini ya kuongezeka kwa utalii. Idara ya Mambo ya Kale nchini Tanzania inafanya kazi ili kudumisha maboma ya zama za kikoloni karibu na Bagamoyo na kuimarisha mji. Mwaka wa 2006, idara hiyo iliomba UNESCO kuingiza Bagamoyo katika orodha ya Urithi wa Dunia (World Heritage), katika jamii ya kitamaduni.

Bandari[hariri | hariri chanzo]

Bandari mpya iitwayo Bagamoyo Port, inajengwa Mbegani, karibu na Bagamoyo. Serikali ya Uchina imewekeza dola la Kimarekani bilioni 10 ili kuifanya bandari hii kuwa moja ya bandari muhimu Afrika.

Wakazi maarufu[hariri | hariri chanzo]

Miji dada[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Vallejo Sister City. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-04-14. Iliwekwa mnamo 2017-17-10.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]