Soko la watumwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
soko la watumwa zanzibar

Soko la watumwa lilikuwa mahali ambapo watumwa wananunuliwa na kuuzwa. Masoko hayo yalikuwa muhimu katika historia ya utumwa, hasa katika biashara ya utumwa ya kwenda Uarabuni na Amerika.

Katika utawala wa Ottoman wakati wa karne ya 14, watumwa walikuwa bidhaa ya biashara katika maeneo maalum ya wauzaji ambayo yaliitwa "Esir" au "Yesir". Kulikuwa na watumwa wa umri wowote na jinsia zote mbili, walikuwa uchi kabisa ili wanunuzi waweze kuwakagua.

Kuanzia miaka ya 1800 hadi 1890, soko la watumwa la Zanzibar lilikubwa kubwa kulizo yote duniani. Kati ya watumwa 2500050000 wa Kibantu waliletwa ili kuuzwa kwenda pwani ya Somalia na sehemu nyingine. Wengi wao walitoka katika makabila ya Wamakua, Wanyasa, Wayao, Wazaramo na Wazigua ambao ni makabila ya Tanzania, Msumbiji na Malawi za leo.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Soko la watumwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.