Majadiliano:Utumwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Utumwa ni hali ya mtu kumilikiwa na mtu mwingine au kufanyiswa kazi bila ruhusa yake na kunyimwa haki zake za msingi.mtu anayemilikiwa anakuwa hana hadhi.

Uislamu na utumwa[hariri chanzo]

Uislamu ulikubali utumwa, hivyo katika nchi zinazofuata dini hiyo utumwa ulichelewa zaidi kufutwa.

Lakini Waislamu walifundishwa masharti fulani kama kuwatendea watumwa vizuri. Walifundishwa pia kwamba ni tendo jema mbele ya Mungu (Allah) kumwacha huru mtumwa.

NB: Hii imekaa kiproganda zaidi. Hakuna chanzo cha maelezo hayo. Zaidi utasoma imeandikwa na jamii inayokinzana kimtazamo. Si kama watu wa Ulaya walikuwa waungwana kiasi hicho kama kuna kesi za kubaguana kusoma huko Marekani hadi miaka ya 1950. Sijaona katika kurani mahali popote imetaja utumwa ni halali zaidi ya tamaa binafsi za wanadamu ni sawa na Wazungu kule Ghana wa dhehebu la Katoliki walivyoweka watumwa katika mabanda ilhali ndani ya mabanda kuna kanisa walienda kumuomba Mungu. Sijui ni Mungu gani ni shida tu. Ukweli kuhusu Utumwa Watu wa Ulaya wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kuwasema vibaya Waarabu kama ndio vinara wa utumwa ilhali wao nao walihitaji watumwa kwa kiasi kikubwa hadi hapo walipofanya mapinduzi ya viwanda wakaona isiwe tabu tena, hawahitaji watumwa. Waliona gharama kubwa kuagiza watumwa kuliko kutumia mashine. --Muddyb Mwanaharakati Longa 17:59, 25 Desemba 2020 (UTC) Reply[reply]