Hukwe Zawose
Hukwe Zawose (Bugiri, alizaliwa mwaka 1940 - Bagamoyo, - 30 Desemba 2003) alikuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa asili kutoka Tanzania, akijulikana zaidi kwa mtindo wake wa kipekee ulioakisi utamaduni wa kabila la Wagogo. Ala alizotumia kwa umahiri mkubwa zilikuwa ilimbal na zeze, huku pia akitumia filimbi kwa ustadi wa hali ya juu.
Kipaji chake cha muziki kiligunduliwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius K. Nyerere, wakati wa ziara yake mkoani Dodoma. Nyerere alivutiwa na uimbaji na uchezaji wa Hukwe, na aliporudi Dar es Salaam, alimwalika Hukwe kujiunga na kikundi cha utamaduni cha Taifa Bagamoyo Players, ambacho kilikuza na kuendeleza sanaa za asili za Kitanzania.
Katika miaka ya 1990 Zawose alirekodi muziki pamoja na Peter Gabriel na kutoa CD kadhaa.
Albamu Kadhaa
[hariri | hariri chanzo]- Tanzania Yetu (1989)
- Mateso (1989)
- The Miracle of the Thumb Piano in Tanzania (1989)
- Chibite (1996)
- Mkuki Wa Roho (2000)
- Assembly (2002)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Hukwe Zawose page Ilihifadhiwa 5 Desemba 2006 kwenye Wayback Machine.
- Hukwe Zawose obituary Ilihifadhiwa 15 Juni 2009 kwenye Wayback Machine.
Sikiliza
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hukwe Zawose kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |