Norwei
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Alt for Norge ("Yote kwa Unowe" ni wito wa kifalme) Kiapo kufuatana na katiba ya 1814 : "Enige og tro til Dovre faller" ("Pamoja na waaminifu hadi milima ya Dovre inaporomoka") | |||||
Wimbo wa taifa: Ja, vi elsker dette landet Wimbo wa kifalme: Kongesangen | |||||
Mji mkuu | Oslo | ||||
Mji mkubwa nchini | Oslo | ||||
Lugha rasmi | Kinowe1 (Bokmål na Nynorsk) | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Harald V Jonas Gahr Støre | ||||
Katiba Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
Kutoka maungano na Uswidi 7 Juni 1905 26 Oktoba 1905 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
385,207 km² (ya 673) {{{percent_water}}} | ||||
Idadi ya watu - 2024 kadirio - 2013 sensa - Msongamano wa watu |
5,550,203[1] (ya 116) 5,136,700 14.4/km² (ya 213) | ||||
Fedha | Krone ya Unowe (NOK )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .no2 | ||||
Kodi ya simu | +47
- | ||||
1Lugha rasmi ya Kinowe inapatikana kwa namna mbili: bokmål zaidi kama lugha ya kimaandishi na Nynorsk zaidi kama lugha ya majadiliano ingawa inaandikwa pia. Lugha ya Kisami ni lugha rasmi katika miji 6 na Kifini katika mji mmoja. |
Unowe (auː Norwe, Norwei; kwa Kinorwei Norge/Noreg; jina rasmi ni Ufalme wa Unoweː Kongeriket Norge kwa Bokmål na Kongeriket Noreg kwa Nynorsk) ni nchi ya Skandinavia katika Ulaya ya Kaskazini.
Imepakana hasa na Uswidi, ila katika ncha ya kaskazini na Ufini na Urusi pia.
Ina pwani ndefu kwenye Bahari ya Kaskazini na ya Atlantiki.
Visiwa vya Svalbard na Jan Mayen katika bahari ya Aktiki ni maeneo ya Norwei.
Pia visiwa visivyokaliwa na watu vya Bouvet katika Atlantiki ya kusini na Peter I katika Pasifiki ya kusini viko chini ya Unowe.
Nchi inadai pia sehemu ya Queen Maud Land katika bara la Antaktika penye kituo cha kisayansi cha Troll.
Mkuu wake kwa sasa ni Mfalme Harald V.
Bunge huitwa Stortinget na wanachama wake huchaguliwa na wananchi kila baada ya miaka minne.
Sikukuu ya taifa ni tarehe 17 Mei, ambapo husherekewa katiba ya Unowe ya mwaka wa 1814.
Miji
[hariri | hariri chanzo]Mji mkuu ni Oslo, wenye wakazi wanaozidi 530,000. Miji mingine mikubwa ni pamoja na Bergen wenye wakazi 230,000 na Trondheim wenye wakazi 150,000; yote miwili imewahi kuwa miji mikuu ya Unowe katika miaka ya mwanzoni.[2]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Nchi ilikaliwa na watu wawindaji-wakusanyaji tangu mwaka 10000 KK hivi.
Katika miaka 3000 - 2500 KK waliingia wakulima wa Kizungu.
Katika karne ya 8 hadi karne ya 10 Norwei ilipeleka mabaharia wake Waviking hadi mbali sana.
Kwa muda mrefu Norwei ilibaki katika muungano na Udani na Uswidi.
Ufalme umekuwa huru tangu mwaka wa 1905.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Unowe ilikuwa nchi maskini ya wakulima na wavuvi, lakini tangu kupatikana kwa mafuta ya petroli baharini imekuwa kati ya nchi tajiri kabisa duniani.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Takriban watu milioni 5.5 wanaishi nchini Unowe. Wengi wao (81.5%) ni Wanorwei asili, jamii ya Wajerumani. Asilimia 18.5 ni wahamiaji au watoto wa wahamiaji wawili (hasa Wapolandi, Walithuania, Wasomali, Wapakistani na Waswidi). Wengi wao sasa wana uraia wa Norwei.
Dini ya kwanza ni Ukristo (74.9%), hasa madhehebu ya Kilutheri (68%), halafu Wakatoliki (3.1%, hasa wenye asili ya Polandi). Hata hivyo wananchi wengi hawajali sana; wanaoshiriki ibada kila wiki ni 2% tu.
Katika dini nyingine, unaongoza Uislamu (3.1%) ulioletwa na wahamiaji kutoka nchi mbalimbali walioongezeka sana kuanzia miaka ya mwisho ya karne ya 20. 21.2% hawana dini yoyote.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Population, 2024-01-01" (kwa Kiingereza). Statistics Norway. 2024-02-21. Iliwekwa mnamo 2024-02-25.
- ↑ "Trondheim - the official website". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-08. Iliwekwa mnamo 2009-09-04.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Wikinews has related news: Norway |
OpenStreetMap has geographic data related to: Norwei |
- Norway.no, Norway's official portal
- Statistics Norway
- State of the Environment Norway
- State of the Environment Norway: About Norway Ilihifadhiwa 13 Agosti 2011 kwenye Wayback Machine.
- Norway entry at The World Factbook
- Norway entry at Encyclopædia Britannica
- Norway Ilihifadhiwa 26 Januari 2016 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Norway.info, official foreign portal of the Norwegian Ministry of Foreign Affairs
- Wikimedia Atlas of Norway
- VisitNorway.com, official travel guide to Norway.
- Norway travel guide kutoka Wikisafiri
- vifanord – a digital library that provides scientific information on the Nordic and Baltic countries as well as the Baltic region as a whole.
- Birdwatching Norway Ilihifadhiwa 8 Desemba 2018 kwenye Wayback Machine.
- National Anthem of Norway
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Norwei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |