Salve Regina
"Salve Regina" (tamka:ˈsalve reˈdʒiːna; maana yake: 'Salamu Malkia') ni utenzi wa Kikristo unaotumika katika liturujia ya Kanisa la Kilatini hasa kama antifona mojawapo ya kumalizia Sala ya mwisho nje ya Kipindi cha Pasaka. Kwa kawaida unatumika pia kumalizia sala ya Rozari[1].
Utenzi huo ulitungwa na mtu asiyejulikana[2] wa Ulaya katika Karne za Kati na ulitumika kwanza kwa lugha ya Kilatini, ingawa kuna tafsiri zake nyingi.
Maneno asili kwa Kilatini
[hariri | hariri chanzo]- Salve, Regina, Mater misericordiæ,
- vita, dulcedo, et spes nostra, salve.
- Ad te clamamus exsules filii Hevæ,
- Ad te suspiramus, gementes et flentes
- in hac lacrimarum valle.
- Eia, ergo, advocata nostra, illos tuos
- misericordes oculos ad nos converte;
- Et Jesum, benedictum fructum ventris tui,
- nobis post hoc exsilium ostende.
- O clemens, O pia, O dulcis Virgo Maria.[3]
Tafsiri ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Salamu Malkia, Mama mwenye huruma,
- Uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu.
- Tunakusihi ugenini hapa,
- Sisi wana wa Eva.
- Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika,
- Bondeni huku kwenye machozi.
- Haya basi, Mwombezi wetu,
- Utuangalie kwa macho yako yenye huruma.
- Na mwisho wa ugeni huu, utuonyeshe Yesu,
- Mzao mbarikiwa wa tumbo lako.
- Ee mpole, ee mwema,
- Ee mpendevu, Bikira Maria.[4]
Miziki yake
[hariri | hariri chanzo]Utenzi huo ulipambwa kwa muziki na Tomás Luis de Victoria, Giovanni da Palestrina, Josquin des Prez, Lassus, Marc-Antoine Charpentier, Louis-Nicolas Clérambault, Alessandro Scarlatti, Antonio Vivaldi, Jan Dismas Zelenka, George Frideric Handel na Franz Liszt.
Franz Schubert alitunga walau miziki saba tofauti. Wengine ni Francis Poulenc, Arvo Pärt na Olivier Latry.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ ""The Rosary: Salve Regina (Hail, Holy Queen)", Godzdogz, Blackfriars, Oxford, October 2, 2014". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-02. Iliwekwa mnamo 2022-01-16.
- ↑ Lawrence Gushee, "Hermannus Contractus [Hermann der Lahme, Hermann von Reichenau]," in The New Grove Dictionary of Music and Musicians, 2nd edition (2001): "Although the most venerable ascriptions to Hermannus – the Marian antiphons Alma Redemptoris mater and Salve regina – have been taken away by most recent scholarship, the true authorship is still, and possibly will be for ever, the subject of controversy."
- ↑ "Salve Regina". Preces-latinae.org. Iliwekwa mnamo 2014-07-10.
- ↑ Misale ya waamini, uk. 1528.