Misale ya waamini
Mandhari
Misale ya waamini (awali: Misale ya waumini) ni kitabu kidogo ambacho kinawaletea Wakatoliki wanaotumia lugha ya Kiswahili matini ya sala na masomo kutoka Biblia ya Kikristo kadiri ya utaratibu wa Misa za Jumapili na sikukuu za kalenda ya liturujia ya mapokeo ya Kiroma.
Mbali na hayo, yanayotokana na vitabu rasmi vya Misale ya altare na Kitabu cha masomo, katika kitabu hicho waumini wanakuta pia sala na ibada nyingine za binafsi.
Ndiyo sababu misale hiyo imetolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania mara nyingi na kusambaa nchini kote na hata nje yake.
Toleo jipya kabisa limetolewa mwaka 2021.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Misale ya waamini kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |