Nenda kwa yaliyomo

Mapenzi ya jinsia moja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya fahari, bendera inayowakilisha watu wa LGBT, wakiwemo wapenzi wa jinsia moja.
Utafiti wa mwaka 2019 (Pew Global Research Poll): Asilimia ya wakazi wanaokubali mapenzi wa jinsia moja yawe halali katika jamii:      0-10%      11-20%      21-30%      31-40%      41-50%      51-60%      61-70%      71-80%      81-90%      91-100%      Hakuna taarifa

Mapenzi ya jinsia moja (kwa Kiingereza: homosexuality) ni mwelekeo wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia ileile. Mwelekeo ukifuatwa unageuka tabia.

Mwelekeo wa kimapenzi humaanisha mihemko ya kimahaba au mivuto ya kimapenzi kwa jinsia fulani. Mwelekeo huo kwa kawaida humfanya mtu kupenda jinsia tofauti na ya kwake (kuwa na mvuto kwa watu wa jinsia nyingine), jambo ambalo linawezesha uzazi kadiri ya maumbile.

Hata hivyo kuna wanawake wanaovutiwa na wanawake wenzao na wanamume wanaovutiwa na wanaume wenzao, mbali ya watu wanaovutiwa na jinsia zote mbili (kwa Kiingereza: “bisexual”), mbali na wale wasio na mwelekeo wowote wala kusikia mvuto wowote wa namna hiyo (kwa Kiingereza: “asexuals”).

Watu wana mang'amuzi tofauti juu ya mwelekeo wao wa kimapenzi. Baadhi wanajitambua kwa muda mrefu kabla hawajaanza uhusiano na wengine. Baadhi hujihusisha na vitendo vya kimapenzi kabla ya kujitambua na kuchukua msimamo juu ya mwelekeo wao. Vivutio vya msingi ambavyo huunda mwelekeo wa kimapenzi wa watu wazima kwa kawaida huibuka katika ubalehe.[1] Wakati huo wengine wanayumba kwa muda fulani katika kujitambua, lakini baadaye wengi wao wanakomaa katika mwelekeo wa kawaida [2]. Wapo wanaotaka hao watoto wapewe mapema dawa za kuzuia ubalehe ili baadaye iwe rahisi kuwafanyia upasuaji wa kubadili vyungo vya uzazi kadiri ya mwelekeo wao kama kwamba mwili ulivyo hauna maana. Serikali za nchi mbalimbali, kama Uswidi, Ujerumani na Uingereza, zimeshatakaza tiba za namna hiyo kwa kuona madhara yake kubwa.

Binadamu, akiwa na akili na utashi, halazimiki wala hapaswi kufuata mielekeo yake yote, bali anatakiwa kuidhibiti, la sivyo ataharibika upande wa afya ya mwili na ya nafsi vilevile, mbali ya kuharibu maisha ya jamii. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na mwelekeo wa kuwazini watoto wadogo, mwingine wa kula kupita kiasi, n.k. Wakifuata mielekeo hiyo ataleta madhara tu. Maadili yanafundisha kufikiri kabla ya kufuata mwelekeo wowote.

Kwa namna ya pekee ulawiti[3] ndiyo njia ya mapenzi iliyo hatari zaidi kwa afya[3][4][5][6][7][8], hasa kwa yule anayefanyiwa, kutokana na ulaini wa tishu za sehemu za mkundu[3][5].

Istilahi

[hariri | hariri chanzo]

Aina kuu za wapenzi wa jinsia moja ni wasagaji, mashoga, wasenge na mabasha. Maneno hayo yanaweza kutumika kwa dhihaka au kwa lengo la kudhalilisha watu wa namna hiyo. Matumizi hayo yanaweza kuathiri vibaya hisia na heshima ya watu hao.

Wasagaji ni wanawake wanaojamiiana na wanawake wengine.[9] Neno hilo linatokana na kitenzi "kusaga".

"Wasenge" na "mashoga" ni takribani visawe: yote mawili huhusu mwanamume anayeingiliwa katika ngono ya jinsia moja.[10][9] Kwa sababu ya majukumu ya kijinsia, mara nyingi huhusishwa kwa upungufu wa uanaume, au mwanamume ambaye angetaka awe mwanamke.[11] Kwa upande mwingine, basha ni mwanamume anayemwingilia shoga.[10][9]

Mara nyingi, mashoga huitana "kaka poa", na hivyohivyo wasagaji huitana "dada poa".[9] Kwa Kiingereza, shoga anaitwa gay. Hapo awali, gay ilimaanisha "furaha", lakini imekuwa na maana ya mwanamume anayeelekea watu wa jinsia yake, huku wanawake wa namna hiyo wakitajwa kuwa lesbians.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Tafiti tofauti kote ulimwenguni zimegundua kuwa mtu 1 hadi 10 kati ya 100 wanavutiwa na watu wa jinsia yao wenyewe.

Ushoga umekuwepo katika jamii na tamaduni nyingi, na pia unasemekana kutokea katika spishi 500 hivi za wanyama.[12]

Moja ya dhihirisho la mapema zaidi ulimwenguni la ushoga kati ya watu ni michoro ya miambani ya Wasan wa Zimbabwe ambayo inaonyesha mahusiano ya jinsia moja. Michoro hiyo ya maelfu ya miaka iliyopita na vilevile ushahidi mwingine wa kihistoria unaonyesha kuwa ushoga umekuwepo katika bara la Afrika tangu kale.

Miongo mingi ya utafiti na uzoefu ya kitabibu imepelekea mashirika ya afya na ya afya ya akili kutamka kuwa mielekeo hiyo si ugonjwa.[13][14][15][16] Shirika la Afya Duniani (WHO) liliondoa ushoga katika orodha yake ya magonjwa ya akili mnamo 1990.[17]

Vyanzo vyake

[hariri | hariri chanzo]

Hakuna makubaliano kati ya wanasayansi juu ya sababu hasa ambazo humfanya mtu kuwa na mwelekeo wa kupenda jinsia ileile ya kwake au kupenda jinsia zote mbili badala ya jinsia tofauti. Hata hivyo, wanasayansi wanakubaliana kwamba chanzo cha mwelekeo wa kimapenzi wa mtu ni muungano changamani wa vipengele vya kibiolojia na kimazingira.[18]

Wanasayansi wengi wanafikiri mwelekeo wa kimapenzi hauwezi kubadilika kwa hiari, utashi, nguvu, au malezi tofauti.[19][20][21]. Hadi leo, hakuna utafiti wa kutosha wa kisayansi kuonyesha kwamba tiba inayolenga kubadili mwelekeo wa mapenzi ya jinsia moja ni salama au inafaa. Kwa kuongezea, uhamasishaji wa matibabu ya mabadiliko unaonekana kuchangia mazingira mabaya kwa wapenzi wa jinsia moja.

Hata hivyo, tafiti mbalimbali zimeonyesha watu hao wana matatizo makubwa ya kiakili [22] [23] au walau wana urahisi mkubwa zaidi wa kupatwa nayo [24][25].

Misimamo ya sheria

[hariri | hariri chanzo]
Mashoga wa Marekani.
Wasagaji wa Marekani.
Sheria za nchi kuhusu ushoga
     Ndoa za jinsia moja      Mahusiano mengine      Laws against expression      Faini au kifungo (haitekelezwi)      Faini au kifungo      Adhabu ya kifo (haitekelezwi)      Adhabu ya kifo

Pengine mashoga, wasagaji na wapenda jinsia zote mbili hukumbana na unyanyapaa, na hata ukatili kwa sababu ya mwelekeo wao wa kimapenzi tofauti na kawaida. Wengine hubaguliwa kwenye shule, vyuo na sehemu zao za kazi, hata wananyimwa huduma za afya na haki, na hupata msaada mdogo kutoka kwa wanafamilia na marafiki.[26] Hali hiyo hufanya iwe vigumu kujitangaza kuwa shoga, msagaji, au mpenda jinsia mbili.

Tatizo hilo la kimataifa ni kubwa zaidi katika nchi nyingi za Afrika. Kituo cha Utafiti cha Pew mnamo 2020 kiligundua kuwa 14% tu ya Wakenya wanaona mapenzi ya jinsia moja yanapaswa kukubalika.[27] Hivyo katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), isipokuwa Rwanda, ngono ya jinsia moja huchukuliwa ni uhalifu na pengine adhabu iliyopangwa ni kifungo cha muda mrefu, ingawa kwa kawaida haitekelezwi. Matokeo yake, wachache tu wako wazi kuhusu mwelekeo wao wa kimapenzi, wakati wengi wanalazimika kuishi kwa usiri na uwongo, ili waendane na maadili yaliyokubalika katika jamii yao.

Chuki dhidi ya mashoga (kwa Kiingereza: “homophobia”) ina madhara makubwa kwa afya ya akili na ustawi wa wasagaji, mashoga na wapenda jinsia mbili, hasa wakijaribu kuficha mwelekeo wao wa kimapenzi. Unyanyapaa na ukatili vinazidisha mafadhaiko waliyonayo tayari kutokana na kutambua tofauti iliyopo kati ya mwili wao na mwelekeo wao. Mara nyingi wanashindwa kukabili hali hiyo na kujikubali walivyo. Hivyo wako katika hatari ya kuingia ulevi wa aina mbalimbali na kujiua kuliko wenzao wanaovutiwa na jinsia tofauti[28]. Watu wanaotamani kuwasaidia wanaweza kufanya kazi na mashirika husika kuwapatia ushauri nasaha[29] pamoja na kupambana na unyanyapaa.

Mashoga, wasagaji na wapenda jinsia mbili wanaotaka kupunguza unyanyapaa wanaweza kuwa wazi kuhusu mwelekeo wao wa kimapenzi, huku wakichukua tahadhari muhimu ili kuwa salama kadiri iwezekanavyo. Kuwaambia watu wengine kuwa wewe ni mpenzi wa jinsia moja au tofauti huitwa “kujitokeza”. Mara nyingi hiyo ni hatua muhimu ya kisaikolojia kwa sababu wanaohisi lazima wafiche mielekeo yao ya kimapenzi huripoti wasiwasi wa mara kwa mara kuliko mashoga na wasagaji ambao wako wazi.[14]

Misimamo ya dini

[hariri | hariri chanzo]

Uyahudi, Ukristo, na Uislamu kimapokeo huchukulia tabia za mapenzi ya jinsia moja kuwa ni dhambi.[30][30][31][32] Mafundisho ya Uhindu, Ubudha, Ujain, na Kalasinga hayako wazi kabisa juu ya mwelekeo wa mapenzi ya jinsia moja, na viongozi wa dini hizo wanatoa maoni tofauti. Leo, watu kutoka dini zote wanazidi kukubali mapenzi ya jinsia moja, na hata ndoa ya jinsia moja. Idadi inayokua ya madhehebu ya Uprotestanti hufanya baraka za ndoa za jinsia moja. Asilimia kadhaa za wapenzi wa jinsia moja wanaripoti kwamba hawaoni mgongano kati ya mwelekeo wao wa kimapenzi na imani yao.

Katika Biblia

[hariri | hariri chanzo]

Kadiri ya Biblia, Mungu baada ya kumuumba Adamu alisema, “Si vema mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (Mwa 2:18). Maana yake, umbile la mwanamume linaelekea kukamilishana na lile la mwanamke kiroho na kimwili. Kwa kuwa roho haionekani, ni rahisi zaidi kuona jinsi miili yao inavyofaa kuungana iwe mwili mmoja. Hata hivyo mkamilishano huo unafanyika katika nafsi pia, ambazo zina vipawa tofauti vinavyowezesha kwa pamoja kukabili vizuri maisha ya nyumbani, ya uchumi, ya siasa, ya dini n.k. Kufikiria uumbaji wa mtu katika jinsia mbili ndiyo njia ya kuelewa Muumba alitaka nini, kwamba jinsia hizo zinalenga kukamilishana katika ndoa kwa kupendana na kuzaliana (Mwa 1:26-28): "Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi".

Kadiri ya Mtume Paulo, kushindwa kutambua kwamba jinsia hizo mbili zinalenga kukamilishana katika ndoa kwa kupendana na kuzaliana ni sawa na kupotewa na hekima[33].

Katika Kanisa Katoliki

[hariri | hariri chanzo]

Papa Fransisko, mkuu wa Kanisa Katoliki, ameongea mara kwa mara juu ya hitaji la kukaribisha na kupenda watu wote, bila kujali mwelekeo wao wa kimapenzi, kwa kuwa wote ni sura na mfano wa Mungu. Hata hivyo mafundisho ya Kikatoliki <ref>The teachings of the Catholic Church on same-sex attraction are summarized in the Catechism of the Catholic Church:

2357 Homosexuality refers to relations between men or between women who experience an exclusive or predominant sexual attraction toward persons of the same sex. It has taken a great variety of forms through the centuries and in different cultures. Its psychological genesis remains largely unexplained. Basing itself on Sacred Scripture, which presents homosexual acts as acts of grave depravity, tradition has always declared that 'homosexual acts are intrinsically disordered.' They are contrary to the natural law. They close the sexual act to the gift of life. They do not proceed from a genuine affective and sexual complementarity. Under no circumstances can they be approved.

2358 The number of men and women who have deep-seated homosexual tendencies is not negligible. This inclination, which is objectively disordered, constitutes for most of them a trial. They must be accepted with respect, compassion, and sensitivity. Every sign of unjust discrimination in their regard should be avoided. These persons are called to fulfill God's will in their lives and, if they are Christians, to unite to the sacrifice of the Lord's Cross the difficulties they may encounter from their condition.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Long, Monique. "Adolescent Sexuality" (kwa Kiingereza). Umoja wa Mataifa. Iliwekwa mnamo 2024-04-07.
  2. http://mygenes.co.nz/mgmmdi_pdfs/Summary.pdf
  3. 3.0 3.1 3.2 Krasner, Robert I (2010). The Microbial Challenge: Science, Disease and Public Health. Jones & Bartlett Publishers. ku. 416–417. ISBN 978-0763797355. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 21, 2021. Iliwekwa mnamo Agosti 28, 2013.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Hales, Dianne (2008). An Invitation to Health Brief 2010-2011. Cengage Learning. ku. 269–271. ISBN 978-0495391920. Iliwekwa mnamo Agosti 29, 2013.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 Hoeger, Werner W. K.; Hoeger, Sharon A. (2010). Lifetime Fitness and Wellness: A Personalized Program. Cengage Learning. uk. 455. ISBN 978-1133008583. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 6, 2021. Iliwekwa mnamo Agosti 28, 2013.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Dianne Hales (2014). An Invitation to Health. Cengage Learning. uk. 363. ISBN 978-1305142961. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 10, 2021. Iliwekwa mnamo Mei 1, 2015.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Leichliter, Jami S (2008). "Heterosexual Anal Sex: Part of an Expanding Sexual Repertoire?". Sexually Transmitted Diseases. 35 (11): 910–911. doi:10.1097/olq.0b013e31818af12f. PMID 18813143. S2CID 27348658.
  8. World Health Organization, Department of Reproductive Health and Research Global strategy for the prevention and control of sexually transmitted infections: 2006–2015. Breaking the chain of transmission Archived Machi 23, 2014, at the Wayback Machine, 2007, ISBN 978-92-4-156347-5
  9. 9.0 9.1 9.2 9.3 Böhme, Claudia (2015). "Showing the Unshowable: The Negotiation of Homosexuality through Video Films in Tanzania". Africa Today (kwa Kiingereza). 61: 63–82 – kutoka JSTOR.
  10. 10.0 10.1 Amory, Deborah P. (1998). Murray, Stephen O.; Roscoe, Will (whr.). Mashoga, Mabasha, and Magai: 'Homosexuality' on the East African Coast. Boy-Wives and Female Husbands (Ripoti) (kwa Kiingereza). uk. 77.
  11. Kashiha, John; Ross, Michael; Rider, Nic (2022). "Distinguishing trans women in men who have sex with men populations and their health access in East Africa: A Tanzanian study". African Journal of Primary Health Care & Family Medicine (kwa Kiingereza). 14.
  12. Bagemihl, Bruce (1999). Biological Exuberance: Animal Homosexuality and Natural Diversity (kwa Kiingereza). St. Martin's Press. ISBN 978-0-312-25377-6.
  13. Victor, Cornelius J; Nel, Juan A; Lynch, Ingrid; Mbatha, Khonzi (2014). "The Psychological Society of South Africa sexual and gender diversity position statement" (PDF). South African Journal of Psychology (kwa Kiingereza). 44 (3): 5–6. doi:10.1177/0081246314533635.
  14. 14.0 14.1 "An Open Statement from the Psychological Society of South Africa to the People and Leaders of Uganda Concerning The Anti-Homosexuality Bill 2009" (PDF) (kwa Kiingereza). Psychological Society of South Africa.
  15. "Submission to the Church of England's Listening Exercise on Human Sexuality" (kwa Kiingereza). The Royal College of Psychiatrists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-10-16. Iliwekwa mnamo 2013-06-13.
  16. "Appropriate Therapeutic Responses to Sexual Orientation" (PDF) (kwa Kiingereza). American Psychological Association. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2010-06-15.
  17. "Stop discrimination against homosexual men and women" (kwa Kiingereza). Shirika la Afya Duniani. 2011-05-17. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-09.
  18. "Sexual orientation, homosexuality and bisexuality" (kwa Kiingereza). American Psychological Association. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-08-08.
  19. "Submission to the Church of England's Listening Exercise on Human Sexuality". The Royal College of Psychiatrists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-10-16.
  20. Frankowski BL; American Academy of Pediatrics Committee on Adolescence (2004). "Sexual orientation and adolescents". Pediatrics (kwa Kiingereza). 113 (6): 1827–32. doi:10.1542/peds.113.6.1827. PMID 15173519. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-03-20.
  21. Gloria Kersey-Matusiak (2012). Delivering Culturally Competent Nursing Care (kwa Kiingereza). Springer Publishing Company. uk. 169. ISBN 978-0826193810. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-11-30. Most health and mental health organizations do not view sexual orientation as a 'choice.'
  22. McNeil, Jay; Bailey, Louis; Ellis, Sonja; Morton, James; Regan, Maeve; Scottish Transgender Alliance; TREC; Traverse: Crossing Boundaries in Research; Sheffield Hallam University; TransBareAll (Septemba 2012). "Trans Mental Health Study 2012" (PDF). .gires.org.uk. Multiple. Iliwekwa mnamo 20 Desemba 2014.
  23. Transgender Equality Network Ireland (TENI) (2 December 2013). Press Release: New survey reveals nearly 80% of trans people have considered suicide (Press release). Transgender Equality Network Ireland (TENI). Archived from the original on 5 March 2016. https://web.archive.org/web/20160305071910/http://teni.ie/news-post.aspx?contentid=970. Retrieved 20 December 2014.
  24. http://mygenes.co.nz/whiteheadcomorbid10_2.pdf
  25. http://mygenes.co.nz/mental_ill.html
  26. Tusipopata Huduma, Tutakufa: Kuandamwa kwa LGBT na Kunyimwa Haki ya Afya Tanzania (Ripoti). Human Rights Watch.
  27. The Global Divide on Homosexuality Persists (Ripoti) (kwa Kiingereza). 2020-06-25. Iliwekwa mnamo 2024-04-10.
  28. http://mygenes.co.nz/suicide.html
  29. https://www.lifesitenews.com/news/ex-gay-threatened-with-jail-time-fines-for-testifying-about-leaving-homosexuality/?utm_source=digest-profamily-2023-01-25&utm_medium=email
  30. 30.0 30.1 Biblia Takatifu Walawi 20:13
  31. "Katekisimu ya Kanisa Katoliki". Iliwekwa mnamo 2024-04-07.
  32. "Do you approach males among the worlds And leave what your Lord has created for you as mates? But you are a people transgressing". — Quran , Surah 26 (165-166)
  33. Waraka kwa Waroma 1:19–27: "19. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. 20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; 21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. 22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; 23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. 24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. 26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao."

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mapenzi ya jinsia moja kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.