Ukatekumeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Batizio katika kanisa kuu la Asti, Italia.


Ukatekumeni (kutoka neno la Kigiriki κατηχούμενος, katēchúmenos, yaani "mtu anayefundishwa", kwa Kiingereza "catechumen") ni kipindi cha malezi ya Kikristo ambacho kinalenga hasa kuandaa watu kwa ajili ya ubatizo.

Kadiri ya Mtaguso wa pili wa Vatikano, uliorudisha katika Kanisa Katoliki taratibu za karne za kwanza Baada ya Kristo, kisha kuchunguza na kunyosha sababu za uongofu wao, waliojaliwa mwanzo wa imani wapokewe kwa ibada maalumu katika ukatekumeni ambao ufuate maagizo mbalimbali ya sheria za Kanisa.

Madhehebu mengine ya Ukristo, ingawa si yote, yana utaratibu wa namna hiyo.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukatekumeni kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.