Tausi (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Tausi (Pavo ) katika sehemu lao la angani
Ramani ya Tausi;

Tausi (kwa Kilatini na Kiingereza Pavo) [1] ni jina la kundinyota dogo kwenye angakusi ya Dunia yetu lililopo kwenye ncha ya anga ya kusini.

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Tausi lipo karibu na ncha ya anga ya kusini na jirani na makundinyota ya Darubini (en:Telescopium) upande wa kaskazini, Ndege wa Peponi (Apus) na Madhabahu (en:Ara) upande wa magharibi, Thumni (en:Octans) upande wa kusini na Mhindi (en:Indus) upande wa mashariki.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Tausi ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa katika enzi ya kisasa. Kama nyota nyingi zinazoonekana kutoka nusutufe ya kusini pekee haikujulikana kwa Wagiriki wa Kale wala kwa Waarabu kwa hiyo wataalamu wa Ulaya hawakuwa na habari nazo. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi Pieter Dirkszoon Keyser na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia ikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika globu ya nyota ya Petrus Plancius na kupokelewa katika ramani za Johann Bayer.

Keyser alitumia jina la Kiholanzi "De Pauww" (Tausi) iliyotajwa baadaye kwa jina la Kilatini „Pavo“.

Leo Pavo - Tausi lipo pia kati ya makundinyota 88 yanayoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [2] Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Tau'.[3]

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Nyota za Tausi ni chache na dhaifu; lakini kuna moja angavu inaitwa Peacock au a Alfa Pavonis yenye mwangaza unaoonekana wa mag 1.94 ikiwa na umbali wa miakanuru 179 kutoka Dunia[4].


Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Pavo " katika lugha ya Kilatini ni "Pavonis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Pavonis, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  3. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  4. [http://stars.astro.illinois.edu/sow/peacock.html Peacock (Alpha Pav), tovuti ya Prof John Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tausi (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.