Mashuke (kundinyota)
Mashuke (pia: Nadhifa) ni kundinyota la zodiaki inayojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la en:Virgo[1].
Nyota za Mashuke huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Mashuke" linaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.
Jina
Mabaharia Waswahiuli walijua nyota hizi zaidi kwa jina la "Nadhifa" (aliye safi) ambalo ni kifupisho cha Kiarabu العذراء النظيفة al-ʿadhraaʾ an-naḍhiifa yaani "bikira safi". Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale. hao walipokea kundinyota hili tayari kutoka Babeli na tangu mwanzo watu waliona uhusianio kati ya nyota hizi na rutba pamoja na miungu wa kike.
Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Nadhifa" halitumiwi tena ikiwa kundinyota linaitwa "Mashuke" na wakati mwingine pia Sumbula. Ila tu "Sumbula" ni jina la nyota angavu zaidi katika kundinyota hili (Spica, au Alfa Virginis). Asili ya "mashuke/ sumbula" ni picha iliyotumiwa kuchora kundinyota hili iliyokuwa binti anayebeba mashuke ya ngano. Waarabu waliopokea kundinyota pamoja na ishara yake kutoka kwa Wagiriki hawakuchora tena mwili wa binti kutokana na kanuni za dini yao walichora mashuke pekee yanayoitwa "sunbula" kwa Kiarabu. Katika mapokeo ya Kiarabu majina ya "nadhifa" na "sunbula" yalitumiwa sambamba.[2]
Mahali pake
Mashuke iko angani kwenye mstari wa zodiaki kati ya Simba, pia Asadi (Leo) upande wa magharibi na Mizani (Libra) upande wa mashariki.
Magimba ya angani
Kuna nyota nyingi katika eneo la kundinyota hii. Inayoonekana na mashuhuri zaidi ni Sumbula (en:Spica) au "Alfa Virginis". Pamoja na nyota nyingine kuna pia magalaksi kadhaa katika Nadhifa. Nyota zake zimegunduliwa hadi 2017 kuwa na sayari za nje 35 zinazozunguka nyota 29 za Nadhifa.
Jina la (Bayer) |
Namba ya Flamsteed |
Jina (Ukia) |
Mwangaza unaoonekana |
Umbali (miakanuru) |
Aina ya spektra |
---|---|---|---|---|---|
α | 67 | Sumbula (Spica ) | 0,98 | 262 | B1 III/IV + B2 V |
ε | 47 | Vindemiatrix | 2,85 | 102 | G8 III |
ζ | 79 | 3,38 | 73 | A3 V | |
δ | Minelauva | 3,38 | ca. 200 | M3 III | |
β | Zavijah | 3,59 | 36 | F8 V | |
γ | 29 | Porrima | 3,48 + 3,50 | 39 | F0 V + F0 V |
109 | 3,73 | 129 | A0 V | ||
μ | 107 | 3,87 | 61 | F2 III | |
η | 15 | Zaniah | 3,89 | 250 | A2 IV |
ν | 3 | 4,04 | 313 | M0 III | |
ι | 99 | Syrma | 4,1 | 70 | F |
ο | 9 | 4,12 | 171 |
Tanbihi
- ↑ Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Virgo" katika lugha ya Kilatini ni "Virginis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Virginis, nk.
- ↑ Allen, Star-names, uk. 464
Marejeo
- Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 460 ff (online kwenye archive.org)
- Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
Viungo vya Nje
- The Deep Photographic Guide to the Constellations: Virgo
- Star Tales – Virgo
- Virgo Constellation at Constellation Guide
- Warburg Institute Iconographic Database (over 400 medieval and early modern images of Virgo) Ilihifadhiwa 24 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
Makundinyota ya Zodiaki Majina ya kisasa yanafuatwa kwa mabano na jina la mabaharia na jina la Kilatini (la kimataifa) |
||
---|---|---|
Kaa (Saratani – Cancer ) • Kondoo (Hamali – Aries ) • Mapacha (Jauza – Gemini ) • Mashuke (Nadhifa – Virgo ) • Mbuzi (Jadi – Capricornus ) • Mizani – Libra ) • Mshale (Kausi – Sagittarius ) • Ndoo (Dalu – Aquarius ) • Nge (Akarabu – Scorpius ) • Ng'ombe (Tauri – Taurus ) • Samaki (Hutu – Pisces ) • Simba (Asadi – Leo ) |