Njiwa (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nyota za kundinyota Njiwa (Columba) katika sehemu yao ya angani

Njiwa (kwa Kilatini na Kiingereza Columba) [1]. ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu. Iko jirani na kundinyota ya Mbwa Mkubwa na Mkuku (lat. Carina).

Jina[hariri | hariri chanzo]

Njiwa ni kati ya kundinyota zilizobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka dunia yote yaani karne ya 16 na wachoraji wa ramani kukamilisha atlasi za nyota. Mnamo mwaka 1612 Mholanzi Petrus Plancius alitenga nyota hizi kutoka kundinyota ya Mbwa Mkubwa [2] na kuzitaja "Njiwa" kwa kumbukumbu ya njiwa iliyotumwa na Nuhu katika masimulizi ya Biblia [3] na kuzichora hivyo katika katika globu ya nyota yake. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni Col[4].

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Nyota angavu zaidi ni Phact au Alpha Columbae yenye mwangaza unaoonekana wa mag 2.7. Hii ni nyota yenye rangi ya buluu-nyeupe iliyo na umbali wa miaka ya nuru 268 kutoka kwetu duniani.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Columba" katika lugha ya Kilatini ni " Columbae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Columbae, nk.
  2. http://www.ianridpath.com/startales/columba.htm Ian Ridpath's Star Tales: Columba, the Dove
  3. ling. Kitabu cha Mwanzo 8, 8-12
  4. Tovuti ya Ukia, The Constellations, iliangaliwa Septemba 2017