Rakisi (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Rakisi (Hercules) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Rakisi-Hercules, kwa macho ya mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia

Rakisi (kwa Kilatini na Kiingereza Hercules) [1] ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia yetu.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Rakisi ni jina lililotumiwa tangu zamani na mabaharia Waswahili waliojua njia yao baharini wakati wa usiku wakiangalia nyota[2]. Jina hili waliwahi kupokea kutoka kwa Waarabu walioiita الرقيس ar-raqiis linalomaanisha "mchezaji". Katika umbo la nyota watu wa kale walimwona mtu anayepiga goti moja au mtu anayechezacheza. Eratosthenes wa Aleksandria alikuwa wa kwanza aliyemtaja kwa jina la mshujaa Herakles wa mitholojia ya Kigiriki[3] lakini ilichukua muda mrefu hadi jina hili lilishinda majina mengine na hivyo aliitwa Hercules kwa Kilatini.

Hercules ilikuwa moja ya makundinyota 48 zilizoorodheshwa na Klaudio Ptolemaio kwa jina la εν γόνασιν en gonasin yaani "mwenye kupiga goti". Ilipokelewa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia katika orodha ya makundinyota 88 za kisasa iliyotolewa mwaka 1930. [4] Kifupi rasmi ni ‘Her’.[5]

Waarabu waliotafsiri orodha ya Ptolemaio waliendelea kumwita ama الجاثي al-jathi "mpiga goti" au رقيس raqis "mchezaji" na hivyo "Rakisi" ilifika kwa mabaharia Waswahili.

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Rakisi - Hercules lipo karibu na nyota angavu ya Vega.

Inapakana na makundinyota jirani za Tinini (Draco), Bakari (Bootes), Kasi ya Masakini (Corona Borealis), Hayya (Serpens), Hawaa (Ophiuchus), Ukabu (Aquila),, i ( Sagitta), . Mbweha ( Vulpecula) na Kinubi (Lyra).

Rakisi - Hercules anakaa juu ya Tinini (Draco) akishindana naye katika hadithi ya mitholojia.

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Nyota za Rakisi - Hercules zilitazamiwa kama mtu anayepiga goti au akicheza

Rakisi - Hercules ni kundinyota kubwa leyenye nyota nyingi lakini si angavu sana.

β Beta Herculis au “Kornephoros" ni nyota angavu zaidi. Ina mwangaza unaoonekana wa 2.77 ikuwa na umbali unaokadiriwa kuwa miakanuru 148[6].


Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
β 27 Beta Herculis au Kornephoros 2,78m 148 G8 III
ζ 40 2,81m 35 G0 IV
α 64 Ras Algethi 3,1 bis 3,7m 384 M5 Ib
δ 65 Delta Herculis au Sarin 3,12m 79 A3 IV
π 67 3,16m 367 K2 III
μ 86 3,42m 27 G5 IV
η 44 Sophian 3,48m 112 G8 III
ξ 92 3,70m 135 G9 III
γ 20 3,74m 193 A9 III
ι 85 3,82m 494 B3 IV
ο 103 3,84m 347 B9 V
θ 91 3,86m 759
τ 22 3,91m 314 B5 IV
ρ 75 4,1m 403 A0 + A0
110 4,19m
σ 35 4,20m 314 B9 V
φ 11 4,23m 204
95 4,3m 418 A5 + G8

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Hercules" katika lugha ya Kilatini ni "Herculis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Herculis, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. ling. Allen 1899: Star-Names and their Meanings
  4. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Oktoba 2017
  5. "The IAU list of the 88 constellations and their abbreviations" ya mwaka 1922, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, iliangaliwa Mei 2017
  6. KORNEPHOROS (Beta Herculis), tovuti ya Prof. Jim Kaler, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 238 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331