Sagita (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Sagita (Sagitta) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Sagita - Sagitta jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kusini

Sagita (kwa Kilatini na Kiingereza Sagitta) [1] ni jina la kundinyota ndogo iliyopo kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia.

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Sagita (Sagitta) lipo karibu na nyota angavu za Vega na Tairi. Inapakana na makundinyota jirani ya Mbweha (Vulpecula), Rakisi (Hercules), Ukabu (Aquila) na Dalufnin (Delphinus)'.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Sagita (Sagitta) lilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema السهم as-sahm kwa maana ya “mshale” [2]. Waarabu walitafsiri hapa jina la Ptolemaio aliyetaja nyota hizi vile kwa jina la Βέλος Velos katika orodha yake ya Almagesti.

Sagitta - Sagita ni kati ya makundinyota 48 yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika kitabu cha Almagesti wakati wa karne ya 2 BK. Lipo pia katika orodha ya makundinyota 88 yaliyorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [3] kwa jina la Sagitta. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'Sge'.[4]

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Nyota angavu zaidi ni Gamma Sagittae. Ina mwangaza unaoonekana wa mag 3.5 ikiwa na umbali wake unakadiriwa kati ya miakanuru 258 kutoka Dunia[5][6].

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
γ 12 3,5m M0 III
δ 7 3,7m M2 II + B6
β 6 4,4m G8 IIIa
α 5 Sham 4,4m -
Habari za mwangaza na umbali vinaweza kubadilika kutokana na vipimo vipya

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Sagitta" katika lugha ya Kilatini ni "Sagittae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Sagittae, nk.
  2. ling. Knappert 1993; anarejelea jina la Kiarabu kuwa "Sahm al Hamsa" yaani "mishale mitano"
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  4. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  5. Sagitta, tovuti ya Constellation Guide, iliangaliwa Oktoba 2017
  6. Gammaa Sagittae, tovuti ya Prof. Jim Kaler

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 131 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331