Saa (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Saa (Horologium ) katika sehemu yao ya angani

Saa (kwa Kilatini na Kiingereza Horologium) [1] ni jina la kundinyota ndogo kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu.

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Saa lipo jirani na makundinyota ya Nahari (Eridanus, yaani mto), Patasi (Caelum), Nyavu (Reticulum), Panji (Dorado [2]) na Nyoka Maji (Hydrus).

Jina[hariri | hariri chanzo]

Saa ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa katika kipindi cha kisasa. Kama ilivyo kwa nyota nyingine zinazoonekana kutoka nusutufe ya kusini pekee haikujulikana kwa Wagiriki wa Kale wala kwa Waarabu kwa hiyo wataalamu wa Ulaya hawakuwa na habari nazo. Kundinyota hii ilielezwa mara ya kwanza na Mfaransa Nicolas-Louis de Lacaille wakati wa karne ya 18 kwa jina “ l'Horloge à pendule & à secondes“ lililomaanisha “ saa yenye timazi na mkono wa sekunde ».

Lacaille alikaa miaka miwili kwenye Rasi ya Tumaini Jema (Afrika Kusini) alipotazama nyota za anga ya kusini ambazo zilianza tu kujulikana na wanaastronomia wa Ulaya wakati ule. Alipima nyota 10,000 akazipanga katika kundinyota na kutunga majina kwa kundinyota mpya 14[3]. Jina la Kifaransa lilitafsiriwa kwa Kilatini na kufupishwa kama "Horologium " (Saa).

Chaguo la jina lilikuwa dalili ya kipindi cha Zama za Mwangaza ambako Lacaille alitumia majina ya teknolojia mpya ya siku zake kwa kutaja nyota, si tena majina ya mitholojia ya kale.

iko kati ya makundinyota 88 yaliyoorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [4] kwa jina la Horologium. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Hor'.[5]

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Nyota angavu zaidi ni Alpha Horologii ambayo ni nyota jitu yenye rangi ya kichungwa. Mwangaza unaoonekana ni mag 3.9 ikiwa na umbali wa miakanuru 115 kutoka Dunia.[6] [7].

Nyota tatu ilitambuliwa kuwa na sayari, pamoja na Iota Horologii ambayo ni nyota kibete njano inayofanana na Jua yenye umbali wa miakanuru 56.0 kutoka Dunia.[6] Ilitambuliwa kuna na sayari moja yenye ukubwa kama Mshtarii inayoizunguka kila baada ya siku 300.

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
α 3.85m 200 K1 III
δ 4.93m
R 4.7 hadi 14.3m 500 M7 III
β 4.98m
Habari za mwangaza na umbali vinaweza kubadilika kutokana na vipimo vipya

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Horologium " katika lugha ya Kilatini ni "Horologii" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Horologii, nk.
  2. inamaanisha samaki ya aina Coryphaena hippurus
  3. Histoire de l'Académie royale des sciences ; taarifa ya Lacaille katika "Historia ya Akademia ya Kifalme ya sayansi", uk. 588, Tovuti ya Bibliothèque nationale de France (BnF), iliangaliwa Julai 2017
  4. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  5. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  6. 6.0 6.1 van Leeuwen, F. (2007). "Validation of the New Hipparcos Reduction". Astronomy and Astrophysics 474 (2): 653–64. Bibcode:2007A&A...474..653V. arXiv:0708.1752. doi:10.1051/0004-6361:20078357. 
  7. Ridpath, Ian. Horologium. Star Tales. self-published. Iliwekwa mnamo 21 January 2017.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Saa (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.