Mbwa Mkubwa (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nyota za kundinyota Mbwa Mkubwa (Canis Maior) katika sehemu yao ya angani

Mbwa Mkubwa (kwa Kilatini na Kiingereza Canis Maior) [1]. ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu. Shira (Sirius) ambayo ni nyota angavu zaidi angani ni sehemu ya Mbwa Mkubwa.

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Mbwa Mkubwa iko karibu kundinyota ya Jabari (en:Orion) kwa upande wa kusini ya ikweta ya anga. Sehemu yake ya mashariki infika kwenye Njia Nyeupe. Kundinyota jirani zake ni Akarabu (Lepus au sungura), Munukero (kundinyota) (Monocerus), Shetri (Puppis) na Njiwa (kundinyota) (Columba).

Jina[hariri | hariri chanzo]

Mbwa Mkubwa ilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[2]

Jina "Mbwa Mkubwa" latokana na mitholojia ya Ugiriki ya Kale iliyoona hapa mbwa anayewinda pamoja na Jabari (Orion) na kumfuata Akarabu (sungura). Baadaye mbwa wa pili alibuniwa na Waroma. [3] na hapo kundinyota hizi mbili ziliitwa Mbwa Mkubwa na Mdogo. Majina haya yalitafsiriwa baadaye moja kwa moja kwa Kilatini kuwa Canis Maior na Minor na baadaye kwa Kiarabu kuwa الكلب الأكبر Al-Kalb al-akbar na al-asgar.

Mbwa Mkubwa ni kati ya kundinyota zilizotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK. Iko pia kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [4] kwa jina la Canis Maior. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'CMa'.[5]


Nyota[hariri | hariri chanzo]

Nyota angavu zaidi ni Shira (α Alfa Canis Maioris) inayojulikana pia kwa jina la kimataifa ya en:Sirius. Hii ni pia nyota angavu zaidi kushinda nyota zote kwenye anga ikiwa na uangavu unaoonekana wa -1.4 mag na umbali wake na dunia ni miaka ya nuru 8.6 (parseki 2.64)

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Canis Maior" katika lugha ya Kilatini ni " Canis Maioris " na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Canis Maioris, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. ling. Allen, Star-Names and their Meanings uk, 117
  4. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  5. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 75 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbwa Mkubwa (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.