Nenda kwa yaliyomo

Hutu Junubi (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Hutu Junubi (Piscis Austrinus) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Hutu Junubi - Piscis Austrinus jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji wa angakaskazi

Hutu Junubi (kwa Kilatini na Kiingereza Piscis Austrinus) [1] ni jina la kundinyota ndogo kwenye angakusi ya Dunia yetu. Ni tofauti na kundinyota Hutu (au Samaki, Piscis).

Mahali pake

Hutu Junubi (Piscis Austrinus) lipo karibu na ikweta ya anga linapakana na makundinyota jirani ya Mbuzi (pia Jadi au lat. Capricornis), Darubini (Microscopium), Kuruki (Grus), Najari (Sculptor) na Ndoo (pia Dalu au lat. Aquarius).

Jina

Hutu Junubi (Piscis Austrinus) ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema الحوت الجنوبي al-ḥuut al-januubiy kwa maana ya “samaki ya kusini” [2]. Waarabu walitafsiri hapa jina la Ptolemaio aliyetaja nyota hizi vile kwa jina la Νότιος Ιχθύς notios ikhthis katika orodha yake ya Almagesti; jina hili lilitafsiriwa pia kwa السمكة الجنوبية as-samaka(t) al-januubiya[3] kwa kuitofautisha na Hutu au Samaki kwenye angakaskazi.

Piscis Austrinus - Hutu Junubi ni kati ya makundinyota 48 yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika kitabu cha Almagesti wakati wa karne ya 2 BK. Iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [4] kwa jina la Piscis Austrinus. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'PsA'.[5]

Nyota

Kuna nyota moja tu ambayo ni angavu hii ni Alfa Piscis Austrini au Kinywa cha Hutu (en:Fomalhaut) [6]. Ina mwangaza unaoonekana wa mag 1.16 ikiwa umbali wa miakanuru 25 na Dunia[7][8].

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(UKIA)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
α PsA Fomalhaut (Kinywa cha Hutu) 1,16m 25,13 A3 V
δ PsA 4,2m 170 G8 III
ε PsA 4,2m 744 B8 V
β PsA 4,3m 148 A1 V
γ PsA 4,4m
η PsA 5,4m
Habari za mwangaza na umbali vinaweza kubadilika kutokana na vipimo vipya

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Piscis Austrinus" katika lugha ya Kilatini ni "Piscis Austrini" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Piscis Austrini, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. PAL - Glossary "PsA", tovuti ya mradi wa "Ptolemaeus Arabus et Latinus (PAL)" wa Bavarian Academy of Sciences and Humanities, iliangaliwa Oktoba 2017
  4. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  5. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy. 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R.
  6. Fomalhaut - Naming Stars, tovuti ya Ukia, iliangaliwa Novemba 2017
  7. Austrinus-constellation/ Piscis Austrinus, tovuti ya Constellation Guide, iliangaliwa Oktoba 2017
  8. Fomalhaut(Alpha Piscis Austrinus), tovuti ya Prof. Jim Kaler

Viungo vya Nje

Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 131 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331