Tanga (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kwa maana mengine ya jina hili angalia hapa Tanga

Nyota za kundinyota Tanga (Vela) katika sehemu yao ya angani

Tanga (kwa Kilatini na Kiingereza Vela) [1]. ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu. Iko jirani na kundinyota ya Mkuku (Carina) na si mbali na Salibu (Crux).

Jina[hariri | hariri chanzo]

Hadi karne 19 kundinyota hii ilitazamiwa kuwa sehemu ya kundinyota kubwa zaidi iliyoitwa Argo Navis, mara nyingi pekee "Navis" (yaani merikebu) iliyokuwa moja ya kundinyota 48 zilizoorodheshwa na Klaudio Ptolemaio. Lacaille alihesabu ndani yake nyota 180 na hivyo alianza tayari kugawa Argo Navis kwa sehemu tatu za Mkuku (Carina), Shetri (Puppis) na Tanga (Vela). Hii ilithibitishwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia katika orodha ya kundinyota 88 za kisasa iliyotolewa mwaka 1930. [2]

“Vela” inataja matanga ya merikebu. Katika Vela hakuna nyota zinazoitwa Alfa au Beta kwa sababu majina haya yaligawiwa kati ya nyota ya Argo Navis yote kufuatana na uangavu.

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Nyota ng'avu zaidi ni Gamma Velorum ambayo inaonekana kama nyota yenye uangavu wa 1.83 mag. Hali halisi hii ni mfumo wa nyota mbalimbali zinazoonekana kwa macho kama nyota 1 lakini ziko tofauti katika darubini.

γ Gamma na λ Lambda Velorum ziliitwa "Suhail" na Waarabu - hili ni jina lilelile kama Suheli (Canopus) katika kundinyota ya Mkuku (Carina). Sababu yake ni ya kwamba Waarabu walitumia jina hili kwa nyota tatu katika kundinyota ya Argos iliyovunjika baadaye. Kwa Lambda Vel pekee UKIA uliamua kutumia jina hili rasmi, lakini Knappert alipata jina hili kati ya mabaharia Waswahili kwa ajili ya nyota angavu zaidi.


Jina la
Bayer
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miaka ya nuru)
Aina ya spektra
γ Suheli (γ Vel) 1.8 1000 B1 IV
δ Alsephina 1.93 80 A1 V
λ Suhail 2.14 hadi 2.30 573 K4 Ib-II
κ Markeb 2.47 540 B2 IV-V
μ 2.69 116 G5 III SB + G2 V

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Vela" katika lugha ya Kilatini (ambayo ni uwingi wa Velum) ni "Velorum" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Gamma Velorum, nk.
  2. "The IAU list of the 88 constellations and their abbreviations" ya mwaka 1922, iliangaliwa Mei 2017
Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia

Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano