Pampu (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Pampu (Antlia) katika sehemu yao ya angani

Pampu (kwa Kilatini na Kiingereza Antlia) [1] ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu.

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Pampu lipo jirani na makundinyota ya Kantarusi (Centaurus) na Salibu (Crux).

Jina[hariri | hariri chanzo]

Pampu ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa katika kipindi cha kisasa. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na Mfaransa Nicolas-Louis de Lacaille wakati wa karne ya 18 kwa jina “Machine Pneumatique“, Kilatini "Antlia Pneumatica" lililomaanisha “pampu ya hewa ». Lacaille alikaa miaka miwili kwenye Rasi ya Tumaini Jema (Afrika Kusini) alipotazama nyota za anga ya kusini ambazo zilianza tu kujulikana na wanaastronomia wa Ulaya wakati ule. Alipima nyota 10,000 akazipanga katika makundinyota na kutunga majina kwa makundinyota mapya 14[2]. Jina lilitafsiriwa kwa Kilatini na kufupishwa kuwa "Antlia" (pampu) na kupokelewa vile na Mwingereza John Herschel katika orodha yake ya nyota.

Chaguo la jina lilikuwa dalili ya kipindi cha Zama za Mwangaza ambako Lacaille alitumia majina ya teknolojia mpya ya siku zake kwa kutaja nyota, si tena majina ya mitholojia ya kale. Kwa chaguo la « pampu ya hewa » alitaka kuheshimu pampu ya kwanza iliyotumiwa kutengeneza hali ya ombwe kwa kuondoa hewa katika chombo.

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Kundinyota la Pampu lina nyota chache na dhaifu. Angavu zaidi ni α Alfa Antliae yenye uangavu wa 4.28 mag ikiwa umbali wa Dunia wa miaka nuru 366. Uangavu wake unafuatwa na ε Epsilon Antliae halafu na ι Iota Antliae.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Antlia" katika lugha ya Kilatini ni "Antliae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Antliae, nk.
  2. Histoire de l'Académie royale des sciences ; taarifa ya Lacaille katika "Historia ya Akademia ya Kifalme ya sayansi", uk. 588, Tovuti ya Bibliothèque nationale de France (BnF), iliangaliwa Julai 2017
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pampu (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.