Nenda kwa yaliyomo

Ndege wa Peponi (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Ndege wa Peponi (Apus) katika sehemu yao ya angani

Ndege wa Peponi (kwa Kilatini na Kiingereza Apus) [1] ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu.

Mahali pake

[hariri | hariri chanzo]

Ndege wa Peponi liko jirani na kundinyota Pembetatu ya Kusini (Triangulum Australe). Pia lipo karibu na Nyota angavu la Rijili Kantarusi.

Ndege wa Peponi linapatikana kati ya makundinyota yaliyobuniwa tangu mabaharia Wazungu walipozunguka Dunia yote katika karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota ya kusini. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi Pieter Dirkszoon Keyser na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika globu ya nyota ya Petrus Plancius.

Keyser alitumia jina la Kiholanzi la De Paradijs Voghel (Ndege wa Peponi, wa paradiso) lililotajwa baadaye na jina la Kigirikiki „Apus“[2] yaani „bila miguu“ kwa sababu wataalamu wa Ulaya waliamini mwanzoni ya kwamba Ndege wa Peponi hawana miguu. Baadaye ndege hawa waliitwa "ndege wa paradiso" kutokana na rangi nyingi za kupendeza walizo nazo. Leo liko kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [3]

Nyota angavu zaidi ni α Alfa Apodis yenye mwangaza unaoonekana wa 3.83 mag .[4] ikiwa umbali wa Dunia wa miakanuru 447 ± 8,[5] .Ni nyota jitu yenye kipenyo mara 48 kuliko Jua [6] na uangavu halisi mara 928 kulio Jua. Halijoto usoni ni 4312 K.[7]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Apus" katika lugha ya Kilatini ni "Apodis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Apodis, nk.
  2. Bayer aliiiandika kwa jina "Apis Indica" inayomaanisha Nyuki wa Uhindi lakini hapa inaonekana alikosea "apis"= nyuki kwa "avis" = ndege. Johannes Kepler aliandika tayari "Avis Indica". Ling. Wagman, Morton (2003). Lost Stars: Lost, Missing and Troublesome Stars from the Catalogues of Johannes Bayer, Nicholas Louis de Lacaille, John Flamsteed, and Sundry Others. Blacksburg, Virginia: The McDonald & Woodward Publishing Company. pp. 30–32. ISBN 978-0-939923-78-6.
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  4. Ridpath, Ian (2001). Stars and Planets Guide. Princeton, New Jersey: Princeton University Press. ku. 76–77. ISBN 0-691-08913-2.
  5. van Leeuwen, F. (2007). "Validation of the New Hipparcos Reduction". Astronomy and Astrophysics. 474 (2): 653–64. arXiv:0708.1752. Bibcode:2007A&A...474..653V. doi:10.1051/0004-6361:20078357.
  6. Pasinetti Fracassini, L. E.; Pastori, L.; Covino, S.; Pozzi, A. (2001). "Catalogue of Apparent Diameters and Absolute Radii of Stars (CADARS) - Third edition - Comments and statistics". Astronomy and Astrophysics. 367: 524. arXiv:astro-ph/0012289. Bibcode:2001A&A...367..521P. doi:10.1051/0004-6361:20000451.
  7. McDonald, I.; Zijlstra, A. A.; Boyer, M. L. (2012). "Fundamental Parameters and Infrared Excesses of Hipparcos Stars". Monthly Notices of the Royal Astronomical Society. 427 (1): 343–57. arXiv:1208.2037. Bibcode:2012MNRAS.427..343M. doi:10.1111/j.1365-2966.2012.21873.x.
  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 336 ff (online kwenye archive.org)