Globu ya nyota

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Globu ya nyota ya Kiajemi ya karne ya 18, inaonesha picha ya Hawaa (Ophiuchus)
Atlasi akibeba globu ya nyota (Globu ya Farnese) ikioneesha kundinyota za Kantarusi (Centaurus) na Shuja (Hydra)

Globu ya nyota (ing. celestial globe) ni tufe inayoonyesha michoro ya nyota na kundinyota usoni wake. Kwa hiyo ni kama ramani ya nyota iliyochorwa juu ya tufe au globu.

Ramani za aina hii zilitengenezwa tangu zamani na mfano wa kale iliyohifadhiwa ni globu ya Farnese ya karne ya 2 BK inayomuonesha shujaa Atlasi anayebeba globu ya nyota kama ishara ya ulimwengu wote mabegani. Globu za aina hii zilikuwa kifaa muhimu cha mafundisho ya astronomia katika karne zilizopita.

Mtazamaji kwa kawaida anahitaji kuwaza ya kwamba yuko ndani ya tufe.

Viungo vya Nje