Mwanafarasi (kundinyota)
Mwanafarasi (Equuleus kwa Kilatini na Kiingereza) [1]. ni jina la kundinyota ndogo ya nusutufe ya kaskazini ya Dunia.
Mahali pake[hariri | hariri chanzo]
Mwanafarasi linapakana na mkundinyota jirani ya Dalufnin (Delphinus), Dalu au Ndoo (Aquarius), Farasi (Pegasus) na Mbweha (Vulpecula). Kundinyota hii iko karibu na nyota angavu sana ya Tairi (Altair).
Jina[hariri | hariri chanzo]
Mwanafarasi dogo sana kwa hiyo hatuna habari ya matumizi yake na mabaharia Waswahili. Lilitajwa tu na Klaudio Ptolemaio kama „sehemu ya Farasi“ ilichorwa kama kichwa cha farasi tu kando la farasi kubwa la Pegasus. Kunda dalili ya kwamba ilibuniwa na Hipparchos wa Nikaia[2]
Waarabu waliipokea hivi na Wagiriki.
Equuleus - Mwanafarasi ni kati ya makundinyota yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK. Iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa kimataifa wa Astronomia kwa jina la Equuleus. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Equ'. [3]
Nyota[hariri | hariri chanzo]
Jina la (Bayer) |
Namba ya Flamsteed |
Jina (Ukia) |
Mwangaza unaoonekana |
Umbali (miaka nuru) |
Aina ya spektra |
---|---|---|---|---|---|
α | 8 | Kitalpha | 3,92m | 186 | G0 III |
δ | 7 | Delta Equulei | 4,49m | 55 |