Tairi (nyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuhusu kifaa kinachotumiwa kwenye gari angalia hapa tairi

Tairi -Altair katika kundinyota Ukabu (Aquila) katika sehemu yao ya angani
Picha ya Tairi -Altair jinsi ilivyopigwa na darubini kubwa ya Mt Palomar, Kalifornia

Tairi (kwa Kiingereza na Kilatini Altair al-tair, pia α Alpha Aquilae, kifupi Alpha Aqu, α Aqu) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Ukabu (Aquila). Ni pia nyota angavu ya 12 kabisa kwenye anga la usiku. Mwangaza unaoonekana ni mag 0.77. Tairi ni sehemu ya Pembetatu ya Kiangazi kwenye angakaskazi.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Tairi ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema النسر الطائر an-nasr al-tair ambalo linamaanisha “ndege aina ya tai anayepuruka” wakitaja ama kundinyota lote au hasa nyota tatu za a = Tairi, b na g. Hii ilikuwa namna yao ya kutafsiri jina la Kigiriki Ἀετός a-e-tos yaani tai walilolikuta kwa Ptolemaio katika kitabu chake cha Almagesti. Wagiriki waliwahi kupokea kundinyota hili kutoka Wababeli ambao waliona hapa pia ndege mkubwa kwenye anga.

Wataalamu wa Ulaya walipokea jina la Kiarabu kwa ajili ya nyota angavu zaidi na hapa walitumia sehemu ya jina “al-tair” pekee. Kwa Kiarabu neno hili linamaanisha “mwenye kurupuka” na kwa kundinyota walitumia tafsiri ya jina la Kigiriki lenyewe kwa Kilatini “Aquila”.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Tairi - Altair ni nyota ya jamii A kwenye safu kuu. Mwangaza unaoonekana ni mag 0.77 na mwangaza halisi ni 2.22. [2]. Umbali wake na Dunia ni miaka nuru 16.7 [3].

Masi yake ni M☉ 1.79 na nusukipenyo chake R☉ 1.58 (vizio vya kulinganisha na Jua letu) [4].

Tairi ni nyota inayozunguka haraka kwenye mhimili wake. Mzunguko mmoja una muda wa saa 9 pekee (kwa kulinganisha: Jua letu linazunguka kwenye mhimili wake katika muda wa siku 25). Kasi kubwa ya mzunguko inabadilisha umbo la Tairi kufanana na mpira unaokazwa, si tufe. Maana kipenyo kwenye ikweta yake iko 20% kuliko kipenyo kwenye ncha zake. [5]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. ling. Knappert 1993
  2. Buzasi al, uk 2
  3. ALTAIR (Alpha Carinae), tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
  4. Buzasi &al, uk 2 kwa kurejea Erspamer & North na Zakhozhaj
  5. tazama Monnier, Jedwali 1

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 59 (online kwenye archive.org)
  • Buzasi, D. L.; Bruntt, H.; Bedding, T. R.; Retter, A.; Kjeldsen, H.; Preston, H. L.; Mandeville, W. J.; Suarez, J. C.; Catanzarite, J.; Conrow, T.; Laher, R. (2005). "Altair: The Brightest δ Scuti Star". The Astrophysical Journal. 619 (2): 1072–1076 (Online hapa)
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Monnier, J. D.; Zhao, M; Pedretti, E; Thureau, N; Ireland, M; Muirhead, P; Berger, J. P.; Millan-Gabet, R; Van Belle, G; Ten Brummelaar, T; McAlister, H; Ridgway, S; Turner, N; Sturmann, L; Sturmann, J; Berger, D (2007). "Imaging the surface of Altair". Science. 317 (5836): 342–345. (Online hapa)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tairi (nyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.