Ngao (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nyota za kundinyota Ngao (Scutum ) katika sehemu yao ya angani

Ngao (kwa Kilatini na Kiingereza Scutum - Shield) [1] ni jina la kundinyota ndogo kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia yetu.

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Ngao iko angani kati ya kundinyota za Kausi (Mshale) (Sagittarius) na Ukabu (Aquila) ikigusana pia na Hayya (Serpens). Iko karibu na ikweta ya anga.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Kundinyota hii haikujulikana kwa mabaharia Waswahili wa Kale wala kwa Waarabu au Wagiriki kwa sababu nyota zake ni hafifu na chache. nNyota zake zilihesabiwa zamani pia kama sehemu ya kundinyota Ukabu. Scutum – Ngao Ilitajwa mara ya kwanza kama kundi la pekee na mwanaastronomia Johannes Hevelius kutoka Danzig (Ujerumani / Poland) . Hevelius aliyeandika kwa Kilatini alichagua jina “Scutum” na hapo alimaanisha ngao ya mfalme wa Poland akitaka kumheshimu baada ya mapigano ya Vienna ya mwaka 1683 ambako jeshi la Poland iliwashinda Waosmani na kuokoa mji mkuu wa Dola Takatifu la Kiroma[2].

Hevelius akiwa mpika pombe na mfanyabiashara tajiri aliyeendelea kushika kwa muda pia uraisi wa mji wake alikuwa hasa maarufu kwa kuangalia na kupima na kuorodhesha nyota pamoja na mke wake Elisabeth Hevelius.

Scutum - Ngao imepokelewa kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [3] kwa jina la Scutum. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Sct'.[4]

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Ngao –Scutum ina nyota chache tu. Nyota angavu zaidi ni Alfa Scuti yenye mag 3.85 ikiwa na umbali wa miaka ya nuru 199 kutoka Dunia[5].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Scutum " katika lugha ya Kilatini ni "Scuti" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Scuti, nk.
  2. Dola Takatifu la Kiroma ilikuwa jina la Milki kubwa iliyojumlisha Ujerumani, Austria na maeneo ya jirani kama vile Italia ya kaskazini n Bohemia kwa miaka 1000.
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  4. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71.
  5. [ http://stars.astro.illinois.edu/sow/alphasct.html ALPHA SCT (Alpha Scuti)], tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ngao (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.