Uhusika milikishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Uhusika milikishi (en:Genitive case) ni istilahi ya sarufi za lugha za Kihindi-Kiulaya na nyinginezo inayotaja hali ya neno, hasa nomino, kuwa na nomino nyingine.

Katika Kiswahili hali kama hii inatajwa kwa kutumia -a kama kiunganishi, kwa mfano "nyumba ya baba"; kwa Kilatini "domus patri" ambako "patri" ni uhusika milikishi wa "pater" (baba). Kiingereza imeshapotewa na uhusika huu, hivyo kinatumia "father's house". Kwa Kijerumani, Kigiriki na lugha za Kibaltiki zinaendelea kutumia uhusika milikishi.

Matumizi yake yanaeleza badiliko la umbo la neno katika majina ya kisayansi pale ambapo majina yametoka katika lugha ya Kilatini au Kigiriki. Mfano ni majina ya nyota. Nyota angavu zaidi katika kundinyota ya "Centaurus" huitwa "Alfa Centauri" ilhali "Centauri" ni uhusika milikishi wa "centaurus". Vile vile "Alfa Leonis" kwa nyota angavu katika kundinyota ya "Leo" ("Simba", taz. Asadi).