Asadi (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nyota za kundinyota Asadi - Simba (Leo) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Asadi - Simba (Leo) jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini

Asadi ni kundinyota ya zodiaki inayojulikana pia kama Simba au kwa jina lake la kimagharibi la Leo[1]. Ni moja ya kundinyota zinazotambuliwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [2]

Nyota za Asadi huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Asadi" inaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina la Kiswahili ni Asadi na linatokana na Kiarabu أسد asad ambalo linamaanisha "simba". Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Λέων le-on "simba" na hao walipokea kundinyota hii tayari kutoka Babeli na Misri ya Kale. [3] [4]

Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Asadi" limesahauliwa ikiwa kundinyota inaitwa kwa tafsiri tu "Simba".

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Asadi iko angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Saratani (Cancer) upande wa magharibi na Nadhifa (Virgo) upande wa mashariki.

Magimba ya angani[hariri | hariri chanzo]

Asadi huwa na nyota nyingi zinazoonekana kwa macho matupu. Nyota nne angavu zaidi zina magnitudi ya kwanza au pili ambazo ni

 • Maliki Junubi[5] (en:Regulus), pia Alfa Leonis ambayo ni nyota nyeupe-buluu yenye uangavu unaonekana wa 1.34, ikiwa na umbali wa miaka ya nuru 77.5 kutoka dunia. Ni nyota pacha inayoweza kutambuliwa kuwa nyota mbili za karibu kwa kutumia darubini ndogo ya mkononi. Jina lake latokana na Kiarabu ملكى malikiy "kifalme" [6] na جنوبى janubi "kusini"; jina la Kilatini "Regulus" linamaanisha "mfalme mdogo".
 • Beta Leonis (en:Denebola) iko upande wa kinyume wa kundinyota na jina la Kimagharibi ni mafupisho ya Kiarabu ذنب‌الاسد dhanab al asad "Mkia wa Simba". Ina uangavu unaoonekana wa 2.23 ikiwa na umbali wa miaka ya nuru 36 kutoka kwa Dunia.[7]
 • Jabuha Asadi[8] (en:Algieba) au Gamma Leonis ni nyota pacha yenye uangavu unaoonekana wa 2.08 ikiwa na umbali wa miaka ya nuru 126 kutoka dunia. Jina lamaanisha ""paji la uso wa simba".
Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miaka ya nuru)
Aina ya spektra
α 32 Maliki Junubi (Regulus) 1,36m 78 B7 V
γ 41 Algieba 2,01m 126 K1 III + G7 III
β 94 Jabuha Asadi (en:Denebola) 2,14m 36 A3 V
δ 68 Zosma 2,56m 58 A4 V
ε 17 2,97m 251 G1 II
θ 70 Chertan 3,33m 170 A2 V
ζ 36 Adhafera 3,43m 260 F0 III
η 30 3,48m 2000 A0 Ib
ο 14 Subra 3,52m 116 A5 V
ρ 47 3,84m 2500 B1 Ib
μ Rasalas 3,88m 133 K2 III
ι 78 3,9m 70 F2 + G3

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Leo" katika lugha ya Kilatini ni "Leonis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Leonis, nk.
 2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
 3. Hinkley, Star-names and their meanings 252f
 4. Rogers, John H. 1998. "Origins of the Ancient Constellations: I. The Mesopotamian Traditions". Journal of the British Astronomical Association. 108 1: 9–28. Bibcode:1998JBAA..108....9R.
 5. ling. Knappert
 6. ling. Richard Hinckley Allen 1899, Star-Names and their Meanings uk. 256; ingawa Waarabu walitumia zaidi jina la qalb-al-asad" yaani moyo wa simba"
 7. Knappert hana jina la Kiswahili kwa nyota hii ingawa "Dhanabu ya Asadi" inawezekana kwa kulingana na "Dhanabu ya Ukabu"
 8. ling. Knappert

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 252 (online kwenye archive.org)
 • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
Lübeck 2012 (96).jpg Kundinyota za Zodiaki Cal zod.jpg

Akarabu (Nge) - Scorpius * Asadi (Simba) - Leo * Dalu (Ndoo) - Aquarius * Hamali (Kondoo) - Aries * Hutu (Samaki) - Piscis * Jadi (Mbuzi) - Capricornus * Jauza (Mapacha) - Gemini * Kausi (Mbuzi) - Capricornus * Mizani - Libra * Nadhifa (Mashuke) - Virgo * Saratani (Kaa) - Cancer * Tauri (Ng'ombe) - Taurus *