Kantarusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Centaurus Constellation chart
Kentaurus - Kantarusi wa mitholojia ya Ugiriki

Kantarusi (Centaurus kwa Kilatini na Kiingereza) ni jina la kundinyota kwenye angakusi ya Dunia yetu.

Lipo jirani na Salibu (en:Crux) likiwa na nyota mashuhuri ya Rijili Kantori (en:Alpha Centauri) iliyo nyota jirani na Jua letu kuliko zote.

Jina

Jina la Kantarusi lilijulikana tangu kale kwa mabaharia Waswahili waliotumia nyota hizo kutafuta njia yao baharini wakati wa usiku.

Asili ya jina ni Kigiriki Κένταυρος Kentauros, au Kilatini chake kiliichoingia katika lugha za Ulaya kama en:Centaurus. Kiarabu kilipokea jina la Kigiriki kwa umbo la قنطورس qantarus na kutoka hapo liliingia katika Kiswahili.

Kantarusi - Kentaurus ni kiumbe katika mitholojia ya Ugiriki ya Kale kinachounganisha mwili wa binadamu na farasi.

Nyota

Kantarusi ni kundinyota kubwa lililo na mbili za nyota angavu sana kwenye anga[1]. Nyota mashuhuri zaidi ni Rijili Kantori inayojulikana pia kwa jina la Bayer Alfa Centauri maana hii ni nyota iliyo jirani zaidi nasi katika anga-nje ikiwa na umbali wa miakanuru 4.3. Pamoja na Hadar (Beta Cent) ambayo ni pia nyota angavu hizi mbili zinadokeza kwa Salibu (Crux). Rijili Kantori na pia Hadar ni nyota maradufu.


B F Majina Mwangaza unaoonekana Miakanuru Aina ya spektra
α Rijili Kantori au Alpha Centauri A+B, Rigil Kentaurus, Toliman, Bungula −0,27m 4,34 G2 V + K1 V
β Hadar au Beta Centauri, Agena 0,61m 525 B1 III
θ 5 Menkent 2,06m 55 K0 III
γ Muhlifain au Gamma Centauri 2,20m 130 A0 + A0

Katika eneo la Kantarusi kuna fungunyota kadhaa; ω Centauri inaonekana kwa macho matupu kuwa doa dogo na kwa darubini tu nyota kadhaa ndani yake zinatambuliwa[2].

Tanbihi

  1. http://www.constellation-guide.com/constellation-list/Centaurus-constellation/
  2. How To Get a Glimpse of Omega Centauri, tovuti ya skyandtelescope.com, blogu ya 19 Februari 2016, iliangaliwa Aprili 2019

Viungo vya NjeScience-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kantarusi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.