Fungunyota

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Fungunyota ya kilimia
Fungunyota tufe yenye jina la kisayansi Messier2 jinsi inavyoonekana kwa darubini

Fungunyota (Kiing. star cluster) ni idadi ya nyota zinazokaa karibu katika anga la ulimwengu. Zinashikwa pamoja kwa nguvu ya graviti yao. [1] Fungunyota maarufu inayoonekana kwa macho ni Kilimia.

Kwa kutumia mitambo ya kisasa wataalamu wa astronomia wamekuta fungunyota maelfu lakini nyingi hazionekani kwa macho matupu au yanaonekana kama nyota ya kawaida tu.

Fungunyota ni tofauti na kundinyota. Katika kundinyota watu wanajumuisha nyota zinazoonekana kukaa karibu na kuwa na umbo maalumu wakitazama anga kwa macho lakini hali halisi nyota hizi hazina uhusiano kati yao wala hazipo pamoja. Nyingine zipo karibu zaidi na Dunia na nyingine zipo mbali mno. Kinyume chake fungunyota ni kundi la nyota zilizopo karibu.


Kwa jumla kuna aina mbili za fungunyota:

  • fungunyota ya kawaida ambako kwa kawaida idadi haizidi mamia kadhaa. Kilimia ni fungunyota ya aina hii lakini ni kati ya nyota sita hadi tisa tu zinazoonekana kwa macho matupu kutegemeana na hali ya anga.
  • fungunyota tufe (ing. globular cluster) ambayo ni makundi ya nyota maelfu hadi milioni zinazokaa karibu kama tufe kubwa. Chache zao zinaonekana kama nyota kwa macho lakini nyingi zimeonekana tu tangu kupatikana kwa mitambo ya utazamaji ya kisasa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. star cluster (astronomy) -- Britannica Online Encyclopedia. britannica.com. Iliwekwa mnamo 7 Aprili 2010.
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: