Dubu Mdogo (kundinyota)
Dubu Mdogo (kwa Kilatini na Kiingereza Ursa Minor) [1]. ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia yetu.
Nyota angavu zaidi ni Kutubu (en:Polaris) iliyotumiwa sana na mabaharia kwa sababu inaonyesha daima upande wa kaskazini.
Mahali pake
Dubu Mdogo lipo karibu na ncha ya anga ya kaskazini; kundinyota la jirani ni Dubu Mkubwa ( Great Bear), Kifausi (Cepheus) na Twiga ( Camelopardalis). Kutokana na mahali pake karibu na ncha ya anga ya kaskazini ni nyota zake za kusini kabisa tu zinazopita ikweta kwa mtazamaji aliye Tanzania.
Jina
Dubu Mdogo ni kati ya makundinyota yaliyo tajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK. Lipo pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [2] kwa jina la Ursa Minor. [3]
Jina Dubu Mdogo linatokana na ara. الدب الأصغر ad-dubb al-ʾaṣghar yaani “dubu mdogo zaidi” na jina hili lilitafsiriwa kutoka Kigiriki Μικρή 'Αρκτος mikre arktos iliyokuwa pia asili ya jina la Kilatini Ursa Minor. Wagiriki wa Kale walipokea kundinyota hii kutoka kwa mabaharia Wafinisia. Mitholojia ya Wagiriki ina hadithi ya Arkas mwana wa kando wa mungu Zeus aliyebadilishwa na babake kuwa dubu na kutumwa angani kama kundinyota.
Nyota
Nyota angavu zaidi ni Kutubu (α Alfa Dubae Minoris) inayojulikana pia kwa jina la kimataifa ya en:Polaris. Nyota hii ipo kikamilifu kwenye ncha ya kaskazini ya anga kwa hiyo nyota za anga ya kaskazini zote zinaizunguka katika muda wa usiku lakini Kutubu inabaki mahali pake bila kuzunguka. Kutubu haionekani upande wa kusini ya ikweta. Ina mwangaza unaoonekana unaochezacheza kidogo mnamo 2 mag.
Nyota angavu ya pili ni Kochab (β Beta Ursae Minoris) inayofika kidogo juu ya upeo wa macho kwa mtazamaji wa Tanzania. Hii ina mwangaza unaoonekana 2.8 mag ikiwa na umbali kutoka dunia wa miakanuru 126.
Jina la (Bayer) |
Namba ya Flamsteed |
Jina (Ukia) |
Mwangaza unaoonekana |
Umbali (miakanuru) |
Aina ya spektra |
---|---|---|---|---|---|
α | 1 | Polaris | 1.94 hadi 2.05 | 430 | F7 Ib-IIv |
β | 7 | Kochab | 2.07 | 126 | K4 IIIvar |
γ | 13 | Pherkad | 3.00 | 480 | A2 II-III |
ε | 22 | 4,21 | 347 | G5 IIIvar | |
5 | 4,25 | 345 | K4 III |
Tanbihi
- ↑ Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Ursa Minor" katika lugha ya Kilatini ni " Ursae Minoris " na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Ursae Minoris, nk.
- ↑ The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
- ↑ Kwa Kiingereza cha Marekani jina la “Little Dipper” imekuwa kawaida; ‘dipper’ inamaanisha kijiko kikubwa kama upawa wa kuchotea supu
Marejeo
Marejeo
- Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 75 ff (online hapa kwenye archive.org)
- Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dubu Mdogo (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |