Nenda kwa yaliyomo

Zeu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Zeus)
Zeu
Kichwa cha sanamu ya Zeu
Mkuu wa miungu
Mungu wa Mbingu na Radi
MakaoMlima Olimpos
AlamaRadi, Tai, Fahali na Mwaloni
MwenziHera
WazaziKronos na Rhea
NduguHestia, Hades, Hera, Poseidon na Demetra
WatotoAres, Athena, Apolo, Artemi, Afrodita, Dioniso, Heba, Herme, Herakle, Helena, Hefesto, Perseo, Minos, Muza Tisa
Ulinganifu wa KirumiJupiter
Ulinganifu wa KietruskiTinia
Ulinganifu wa KinorsiOdin

Zeu (pia Zeus kutoka Kigiriki: Ζεύς Zeus) ni mkuu wa miungu katika dini ya Ugiriki ya Kale. Analingana na Jupiter katika dini ya Roma ya Kale. Katika imani ya Wagiriki alikalia kilele cha mlima Olimpos pamoja na miungu wenzake alkini alikuwa mkuu na mwenye nguvu kushinda wengine.

Katika masimulizi ya Wagiriki alikuwa mtoto wa miungu Kronos na Rhea na mdogo wa Hestia, Demeter, Hera, Hades na Poseidon. Huyu baba-mungu Kronos alimeza watoto wake wote mara baada ya kuzaliwa akihofia ya kwamba watampindua sawa jini yeye mwenyewe aliwahi kumpindua babake mungu Uranos. Zeu alipoelekea kuzaliwa mamake Rhea alimficha pangoni akampa Kronos badale yake jiwe lililofunikwa na nguo akameza. Zeu alikua haraka akawa mkubwa na hapo alitumia mbinu wa dawa kumlazimisha baba kutapika watoto wote aliowahi kumeza. Baadaye aliungana na wakubwa zake na pamoja walimshambulia Kronos na kumshinda. Sasa miungu waliamua kugawana madaraka; Zeu alikuwa mungu mkuu wa mbinguni, Poseidon mkuu wa bahari na vilindi vyake na Hades mkuu wa dunia ya chini.

Zeu alimwoa dadake Hera akazaa watoto naye lakini alitoroka mara kwa mara kufanya mapenzi na miungu wa kike wengine au na mabinti wa kibinadamu; mitholojia ya Wagiriki ilitaja zaidi ya majina 30 ya miungu au mabinti aliozaa nao.

Aliheshimiwa na Wagiriki wote na kuabudiwa katika mahali pa pekee; pamoja na mahekalu kulikuwa na sehemu za misitu penye miti iliyotazamiwa kuwa miti mitakatifu yake. Kisiwani Kreta waliabudu kwenye mipango aliposemekana kufichwa na mamake.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.