Kronos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kronos akishika mundu aliyotumia kumhatinisha babake Uranos

Kronos alikuwa mungu katika dini ya Ugiriki ya Kale aliyekuwa mkuu wa miungu na mtawala wa ulimwengu katika kipindi kabla Zeus na miungu ya Olimpi.

Kronos alikuwa mwana wa mwisho wa Uranos na Gaia na kwa kufuata ushauri wa mamake Gaia alimhatinisha babake Uranos kwa mundu. Baadaye aliogopa ya kwamba mmoja wa watoto wake angempindua pia hivyo alimeza watoto wake aliyezaa na dadake na mke Rhea. Mwishoni Rhea alifauli kumficha mwana wake wa mwisho Zeus maana wakati Kronos alitaka kummeza Zeus alipewa jiwe iliyoviringishwa katika vitambaa vya mtoto na kuimeza.

Zeus alimpindua babake baadaye akamfunga na kumfukuza mbinguni akamtuma kutawala juu ya kisiwa cha heri.

Baadaye Waroma wa Kale walimtazama kama jina tofauti kwa mungu wao Saturnus.