Visasili vya Kigiriki
Mandhari
(Elekezwa kutoka Mitholojia ya Wagiriki)
Viasili vya Kigiriki ni jumla ya visasili vya Ugiriki ya Kale, yaani ukusanyaji wa masimulizi na hadithi kuhusu vyanzo, miungu na mashujaa wao. Ilikuwa moja ya sehemu za dini ya Ugiriki ya Kale.
Chanzo kikuu kuhusu imani ya Wagiriki wa kale kabisa ni shairi la Theogonia lililotungwa na Hesiodo mnamo mwaka 700 KK.
Nasaba ya miungu ya Titani
[hariri | hariri chanzo]Watitani ni nasaba ya kwanza ya miungu katika visasili vya Kigiriki. Kiasili ni Watitani 12, wakiwemo 6 wa kiume na 6 wa kike wanaofunga ndoa kati yao na kuzaa Watitani wengine. Mkuu wao alikuwa Kronos hadi alipopinduliwa na mwanawe Zeus aliyeanzisha nasaba ya pili ya miungu ya Olimpos. Sehemu ya Watitani walijaribu kumpinga Zeus wakafukuzwa mbinguni.
- Hyperion – mungu wa nuru na jua, aliyemzaa mungu wa jua Helios, mungu wa kike wa mwezi Selene na mungu wa kike wa mapambazuko Eos
- Iapetos – mume wa Klymene (binti wa Okeanos), aliyefukuzwa baadaye mbinguni
- Koios, aliyefukuzwa baadaye mbinguni
- Kreios – mume wa Eurybia
- Kronos – mkuu wa Watitani, baba wa Zeus, mume wa Rhea; alipinduliwa na Zeus akafukuzwa mbinguni akitawala kisiwa cha heri
- Mnemosyne – mama wa Muzi tisa
- Okeanos – mkuu wa bahari na himaya ya maji, baba wa miungu yote ya mito na pepo wa bahari na visima
- Phoibe – mke wa Koios, mungu wa mwezi
- Rhea – mama wa Hestia, Demeter, Hera, Hades, Poseidon na Zeus; alimfuata mumewe Kronos alipoondoka mbinguni
- Themis – mungu wa kike wa haki na mke wa pili wa Zeus; anajua wakati ujao
- Tethys – mke wa Okeanos
- Theia – mke wa Hyperion
Miungu Kumi na Miwili ya Olimpos
[hariri | hariri chanzo]Jina la Kigiriki | Jina la Kiswahili | Maelezo |
---|---|---|
Aφροδίτη (Afrodítē) | Afrodita | Mungu wa kike wa upendo na uzuri. |
Aπόλλων (Apóllōn) | Apolo | Mungu wa nuru na ushairi. |
Άρης (Árēs) | Ares | Mungu wa vita. |
Άρτεμις (Ártemis) | Artemi | Mungu wa kike wa uwindo. |
Αθηνά (Athēná) | Athena | Mungu wa kike wa elimu na hekima. |
Δημήτηρ (Dēmḗtēr)
Δήμητρα (Dḗmētra) |
Demetra | Mungu wa kike wa mimea na kilimo. |
Διόνυσος (Diónysos) | Dioniso | Mungu wa divai. |
Έρως (Érōs) | Ero | Mungu wa mapenzi. |
ᾍδης (Ádēs) | Hade | Mungu wa kuzimu na bwana wa waliokufa. |
Ήφαιστος (Ḗfaistos) | Hefaisto | Mungu wa uhunzi. |
Ήρα (Ḗra) | Hera | Mungu wa kike wa ndoa na malkia ya miungu. |
Ερμής (Ermḗs) | Herme | Mjumbe wa miungu. |
Ἑστία (Estía) | Hestia | Mungu wa kike wa moto. |
Ποσειδῶν (Poseidṓn)
Ποσειδώνας (Poseidṓnas) |
Poseidoni | Mungu wa bahari. |
Ζεύς (Zeús)
Δίας (Días) |
Zeu | Mungu wa radi na mfalme wa miungu. |
Protogenoi
[hariri | hariri chanzo]Jina la Kigiriki | Jina la Kiswahili | Maelezo |
---|---|---|
Αιθήρ (Aithḗr) | Aitheri | Mungu wa anga. |
Ἀνάγκη (Anágkē) | Ananka | Mungu wa kike wa kudra. |
Έρεβος (Érevos) | Erebo | Mungu wa giza. |
Γαία (Gaía) | Gaya | Mungu wa kike wa ardhi. |
Ημέρα (Ēméra) | Hemera | Mungu wa kike wa mchana. |
Χάος (Kháos) | Khaos | |
Χρόνος (Khrónos) | Khrono | Mungu wa muda. |
αἱ Nῆσοι (ai Nḗsoi) | Visiwa | Miungu ya kike wa visiwa. |
Νύξ (Nýx) | Niksi | Mungu wa kike wa usiku. |
Ουρανός (Ouranós) | Urano | Mungu wa mbingu. |
Ούρος (Oúros) | Milima | Miungu ya milima. |
Πόντος (Póntos) | Ponto | Mungu wa bahari ya dunia nzima. |
Τάρταρος (Tártaros) | Tartaro | Mungu wa tartaro. |
Θάλασσα (Thálassa) | Thalasa | Malkia wa bahari na mke wa Ponto. |
Titani Kumi na Wawili
[hariri | hariri chanzo]Jina la Kigiriki | Jina la Kiswahili | Maelezo |
---|---|---|
Ὑπερίων (Yperíōn) | Hiperioni | Mungu wa nuru ya jua. |
Ἰαπετός (Iapetós) | Yapeto | |
Κοῖος (Koïos) | Koyo | Mungu wa fahamu. |
Κρεῖος (Kreïos) | Kreyo | |
Κρόνος (Krónos) | Krono | Mfalme wa Titani. |
Mνημοσύνη (Mnēmosýnē) | Mnemosina | Mungu wa kike wa kumbukumbu. |
Ὠκεανός (Ōkeanós) | Okeano | Mungu wa bahari kuu. |
Φοίβη (Foívē) | Foiba | |
Ῥέα (Réa) | Rea | Malkia wa Titani na mke wa Krono. |
Τηθύς (Tēthýs) | Tethi | Mungu wa kike wa mito. |
Θεία (Theía) | Theya | Mungu wa kike wa uonaji. |
Θέμις (Thémis) | Themi |
- Hekatonkheire (Ἑκατόγχειρες) — majitu yenye mikono mia na miungu wa dhoruba na vimbunga.
- Briareo (Βριάρεως)
- Coto (Κόττος)
- Gige (Γύγης)
- Siklopsi (Κύκλωψ) - majitu-chongo watatu.
- Arge (Ἄργης)
- Bronte (Βρόντης)
- Sterope (Στερόπης)
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |