Nenda kwa yaliyomo

Hesiodo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Hesiodo katika mozaiki ya Kiroma, mnamo karne ya 4 BK
Hesiodi Ascraei quaecumque exstant, 1701

Hesiodo (gir. Ἡσίοδος Hesiodos) alikuwa mshairi mashuhuri wa Ugiriki ya Kale. Pamoja na kazi za Homeri mashairi yake ni misingi wa elimu yetu juu ya vyanzo vya utamaduni wa Ugiriki.

Hesiodo aliishi katika Bootia, Ugiriki ya kati alipokuwa mfugaji wa ng'ombe na mkulima. Mamake aliitwa Pykimede alikuwa na kaka mmoja Perses.

Kati ya mashairi yake yaliyohifadhiwa ni

  • Kazi na siku (gir. Ἔργα καὶ ἡμέραι erga kaì hemerai) anapoeleza mengi kuhusu kazi ya wakulima wa siku zake, pamoja na kusimulia visasili vya Prometheus na Pandora.
  • Theogonia (gir. Θεογονία theogonia; theo= mungu na gonia=kuzaliwa) au shairi linalosimulia jinsi gani miungu ilitokea tangu mwanzo wa dunia.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: