Kimbunga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kwa lugha ya Kimbunga tazama Kimbunga (lugha)
Kimbunga ya "Katrina" juu ya Ghuba ya Meksiko - picha kutoka chombo cha angani tar. 28 Agosti 2005
Picha ya rada ya kimbunga upande wa kaskazini ya ikweta inaonyesha mwendo wake

Kimbunga ni dhoruba kali inayoanza juu ya bahari katika maeneo ya tropiki yenye upepo mwenye kasi ya zaidi ya 117 km/h. Kimbunga ni dhoruba aina ya tufani.

Inaanza juu ya bahari ya kitropiki penye maji yenye halijoto juu ya 26 °C. Hewa joto yenye mvuke nyingi inaanza kupanda juu na kuzunguka. Mzunguko huo unaongezeka kasi kuwa dhoruba. Kasi ikifikia mwendo wa 117 km/h inaitwa kimbunga.

Vimbunga vinatokea katika bahari zote penye maji ya moto kaskazini na kusini ya ikweta. Mzunguko hufuata mwendo wa saa kama kimbunga kinatokea kusini ya ikweta; ni kinyume cha mwendo wa saa kama kinatokea kaskazini ya ikweta.

Kila sehemu ya dunia kimbunga kina jina lake na majina haya yameanza kutumiwa kimataifa:

Hatari za Kimbunga[hariri | hariri chanzo]

Kimbunga inaweza kusababisha hasara kubwa ikigusa meli baharini na zaidi mwambaoni inapofikia nchi kavu au visiwa.

Hatari zake ni hasa kasi ya upepo pamoja na kiasi kikubwa cha mvua. Kasi ya upepo inaweza kuinua vitu vizito kama miti, paa za nyumba au magari na kuvirusha mbali. Watu huuawa na mali kuharibiwa. Uwingi wa mvua husababisha mifuriko.


Majina ya Vimbunga[hariri | hariri chanzo]

Vimbunga hutokea mara kwa mara katika kipindi cha joto. Wataalamu wameanza kuvipa majina kwa kurahisisha maelewano. Katika eneo la kila bahari kuna utaratibu wa pekee wa kutolea majina kwa vimbunga kufuatana na mapatano ya wanasayansi.

Atlantiki inaona takriban vimbunga kumi au zaidi kila mwaka. Hupewa majina kufuatana alfabeti. Imekuwa kawaida tangu 1979 kutumia majina ya kiume na ya kike kwa kubadilishana (zamani vilipewa majina ya kike tu lakini wanawake walilalamika).

Wataalamu wanatumia orodha sita ya majina hivyo jina linaweza kurudia baada ya miaka sita.

Kimbunga ya "Katrina" kilichoharibu mji wa New Orleans katika Agosti 2005 kilikuwa kimbunga cha 11 cha mwaka 2005. Kilifuata kimbunga "Jose" na kufuatwa na "Lee" halafu "Maria". Kama kimbunga inasababisha uharibifu mkubwa sana jina lake huondolewa katika orodha maana yake jina hili halitarudia. "Katrina" imebadilishwa kuwa "Katia" katika orodha ya mwaka itakayotumika mwaka 2011 (ikitokea itakuwa kimbunga kinachofuata "Jose" ya 2011)