Namba za Flamsteed

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Namba za Flamsteed

Namba za Flamsteed (ing. Flamsteed designation) ni utaratibu wa kutaja nyota uliobuniwa na Mwingereza John Flamsteed aliyekuwa mkurugenzi wa kwanza wa paoneaanga pa Greenwich (Royal Greenwich Observatory).

Katika orodha yake nyota zinatajwa kwa namba na kundinyota. Kwa njia hii aliweza kutaja kwa namna ya pekee karibu kila nyota inayoonekana kwa macho matupu.

Mfumo wa Flamsteed unafanana na mfumo wa Bayer aliyetumia jina la kundinyota pamoja na herufi za Kigiriki kwa mfano Alfa Centauri akipata matatizo katika makundinyota makubwa ambayo idadi ya nyota inazidi idadi ya herufi za Kigiriki. Hapo mfumo wa Flamsteed haukuwa na mipaka kutaja hata nyota nyingi.

Flamsteed alitumia uhusika milikishi (en:genitive) wa jina la Kilatini ya kundinyota akiongeza namba (Mfano: Centaurus - uhusika milikishi "Centauri").

Siku hizi namba za Flamsteed zinatumiwa pamoja na majina ya Bayer hasa pale ambako zinahusu nyota ambazo Bayer hakutolea majina, kwa mfano kwa sababu Bayer aliorodhesha 1,564 nyota pekee zinazoonekana kwa macho matupu ilhali Flamsteed alitumia darubini na hivyo aliorodhesha nyota 2,554. Mara nyingi namba za Flamstee zimekuwa kawaida pale ambako Bayer alilazimishwa kuongeza herufi za Kilatini au namba kwa zile za Kigiriki kutokana na idadi ya nyota katika kundinyota fulani. Kwa mfano namba ya Flamsteed "55 Cancri" hupendelewa na jina la Bayer "Rho-1 Cancri".

Marejeo[hariri | hariri chanzo]


http://galileo.rice.edu/Catalog/NewFiles/flamsted.html