Hayya (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya sehemu mbili za kundinyota Hayya (Serpens), jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini

Hayya (kwa Kilatini na Kiingereza Serpens) [1]. ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia yetu.


Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Hayya - Serpens iko katika ukanda wa Njia Nyeupe.

Hii ni kundinyota ya pekee inayopatikana angani kwa sehemu mbili za pekee zinazotengwa na kundinyota ya Hawaa (Ophiuchus). Sehemu mbili zinaitwa Serpens Caput (kichwa cha Hayya au nyoka) upande wa magharibi na Serpens Cauda (Mkia wa Hayya au nyoka) upande wa mashariki. Katikati ya pande hizi mili iko Hayya au Ophiuchus anayetazamia kuwa anabeba nyoka.

Sehemu ya Kichwa cha Hayya (Serpens Caput) inapaka na kundinyota jirani za Mizani (Libra), Nadhifa (Virgo), Bakari (Bootes), Kasi ya Masakini (Corona Borealis), Hawaa (Ophiuchus) na Rakisi (Hercules).

Ng'ambo ya Hawaa iko sehemu ya pili Mkia wa Hayya na hii inapakana na Kausi (Mshale) (Sagittarius), Ngao (Scutum), Ukabu (Aquila) na Hawaa (Ophiuchus).

Jina[hariri | hariri chanzo]

Hayya (Serpens) ilijulikana vile kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2].

Serpens - Hayya ni kati ya kundinyota zilizotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK. “Serpens” au Hayya inataja nyoka mkubwa anayeshikwa na Hawaa (Ophiuchus). Katika mitholojia ya Kigiriki huyu alikuwa Asklepios, mungu wa tiba na nyoka ilikuwa ishara ya nguvu ya dawa linaloweza kuua na kupona.

Hayya iko pia kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [3] kwa jina la Serpens. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Ser'.[4]

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Hayya - Serpens ni kundinyota kubwa yenye nyota nyingi. Unukalhai au α Serpentis ni nyota angavu zaidi iliopo katika sehemu za Caput Serpentis. Ni jitu jekundu lenye mwangaza unaoonekana wa mag 2.6 ikiwa na umbali wa miaka ya nuru 73 na Dunia[5][6].

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miaka ya nuru)
Aina ya spektra
α 24 Unukalhai, Unuk al Hay, Unuk, Cor Serpentis 2,63m 73 K2 III
η 58 3,23m 62 K0 III-IV
μ 32 3,54m 156 A0 V
ξ 55 3,54m 105 F0 IIIp
β 28 Beta Serpentis au Chow 3,65m 153 A3 V
ε 37 3,71m 70 A2 Vm
γ 41 3,85m 36 F6 V
θ1,2 63 Alya 4,03m 132 A5 V

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Serpens" katika lugha ya Kilatini ni "Serpentis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Serpentis, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  4. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71.
  5. Serpens], tovuti ya Constellation Guide, iliangaliwa Oktoba 2017
  6. Unukalhai (Alpha Serpentis), Tovuti ya Prof. Jim Kaler

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 63 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331