Nenda kwa yaliyomo

Asklepios

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Asklepios akishika fimbo ya nyoka
Bendera ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inaonyesha fimbo ya Asklepios

Asklepios (kwa Kilatini: Askulapius) alikuwa nusu mungu katika mitholojia ya Kigiriki. Alitazamiwa ni mwana wa Apollo na mama wa kibinadamu. Alikuwa mungu wa dawa na tiba.

Katika masimulizi ya Wagiriki Asklepios alijifunza siri za tiba kutoka babake mungu Apollo (mungu mlezi wa sanaa na elimu yote pamoja na tiba). Alitembea duniani akawa mganga mashuhuri. Alipofaulu kumfufusha mtu aliyekufa tayari Hades (mungu wa kuzimu) alilalamika juu yake kwa baba wa miungu Zeus na hapo Zeus alimwua Asklepios.

Miji mbalimbali ilikuwa na mahekalu ya Asklepios yaliyokuwa pia vitovu vya elimu ya tiba iliyopatikana nyakati za kale. Asklepios alionyeshwa mara nyingi katika sanamu na picha akionekana kama mwanaume mwenye ndevu anayeshika fimbo lililoviringishwa na nyoka. Fimbo hili la Asklepios hadi leo ni ishara ya tiba, mahali pengi linaonekana kwenye maduka ya dawa. Liko pia katika bendera ya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Farnell, Lewis Richard. Greek Hero Cults and Ideas of Immortality, (Oxford Clarendon Press, 1921).
  • Grimal, Pierre, The Dictionary of Classical Mythology, Wiley-Blackwell, 1996, pp. 62–63 ISBN|978-0-631-20102-1.
  • Hart, Gerald D. MD. Asclepius: The God of Medicine (Royal Society of Medicine Press, 2000)
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.