Ikweta ya anga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ikweta ya anga, Ekliptiki na Mhimili wa Dunia.

Ikweta ya anga (en:celestial equator) ni mstari wa kudhaniwa kwenye anga inayotumiwa katika astronomia. Ni duara kubwa kwenye tufe la anga iliyopo juu ya ikweta ya Dunia. Ni kama pacha ya ikweta ya Dunia angani. [1]

Kutokana na mwinamo wa mhimili wa mzunguko wa Dunia kuna pembe ya nyuzi 23.4° kati ya ikweta ya anga na bapa la ekliptiki.

Mtazamaji anayekaa kwenye ikweta ya Dunia (kwa mfano Nanyuki, Kenya) ikweta ya anga iko juu kabisa. Kwa mtazamaji kwenye ncha za Dunia ikweta ya anga ni sawa na upeo wa macho.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Celestial Equator. Iliwekwa mnamo 5 August 2011.