Mhimili wa mzunguko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Tufe linazunguka kwenye mstari wa kudhaniwa ambao ni mhimili wake wa mzunguko

Mhimili wa mzunguko ni mstari mnyoofu wa kudhaniwa ambako gimba linazunguka.

Katika mfano wa gurudumu mhimili wa mzunguko ni sawa na ekseli.

Kwa magimba ya angani kama Dunia yetu mhimili wa mzunguko ni mstari wa kudhaniwa unaopita kwenye ncha mbili za kaskazini na kusini ukipita kitovu cha masi yake.