Pampu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa kundinyota angalia hapa Pampu (kundinyota)

Pampu sahili ya mkononi: pistoni inaongeza nafasi ndani ya silinda, maji ya chini hufuata upungufu wa shinikizo na kupanda juu

Pampu ni kifaa kinachopeleka kiowevu kutoka mahali pamoja kwenda mahali pengine.

Mfano wa kila siku ni pampu ya mafuta kwenye kituo kinachovuta mafuta, petroli au diseli kutoka tangi hadi gari. Mfano mwingine ni pampu ya maji inayovuta maji kutoka shimo la kisima hadi mdomo wake au moja kwa moja hadi ndani ya nyumba.

Kuna aina mbalimbali za pampu zinazotumia mifumo tofauti.

  • Pampu za skrubu ni kati ya pampu za kwanza zilizojulikana katika historia. Zinatumia mfumo wa skrubu ya Archimedes.
  • Pampu sahili mara nyingi ni pampu ambako pistoni inasukumwa juu ndani ya silinda ya pampu na hivyo kusababisha kupungukiwa kwa shinikizo ya hewa ndani ya silinda. Maji hufuata shinikizo ya duni na kupanda juu.
  • Mfano mwingine wa pampu hutumia mwendo wa mikono inayozunguka ndani ya chemba ya pampu.
  • Moyo wa kibinadamu ni aina ya pampu pia inayotumia mfumo wa kukaza chemba chake na kukipanusha.

Kila pampu inahitaji nguvu fulani inayoendesha kazi yake. Pampu sahili zinaendeshwa kwa nguvu ya kibinadamu au ya wanyama. Tangu kale nguvu ya upepo au ya mwendo wa maji mtoni ilitumiwa pai kuendesha pampu. Haja ya kupata nguvu kwa pampu kwenye migodi ilikuwa sababu ya kugunduliwa kwa injini ya mvuke. Siku hizi pampu nyingi zinaendeshwa kwa nguvu ya umeme.