Suheli ya Tanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Suheli (γ Vel))
Suheli ya Tanga (Gamma Velorum, Regor / Suhail al Muhlif )
Suheli ya Tanga (Regor / Suhail al Muhlif ) katika kundinyota lake la Tanga (Vela)
Kundinyota Tanga (Vela)
Mwangaza unaonekana 1.7
Kundi la spektra A: WC8 + O P: K4 V B: B1 IV
Paralaksi (mas) 2.92
Umbali (miakanuru) 1096
Majina mbadala CD −46° 3847, FK5 309, HD 68273, HIP 39953, HR 3207, SAO 219504, WR 11


Suheli ya Tanga (kwa Kilatini na Kiingereza-Kiarabu Regor / Suhail al Muhlif, pia γ Gamma Velorum, kifupi Gamma Vel, γ Vel) ni nyota angavu zaidi kwenye kundinyota la Tanga (Vela).

Jina[hariri | hariri chanzo]

Nyota ya Suheli katika kundinyota la Tanga ilijulikana na mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka Waarabu wanaoijua kama سهيل المحلف suhail al-muhalaf kwa maana ya “Suhail ya kiapo”; Suhail inayotokana na neno سَهُلَ sahula “tambarare, isiyo na matata” ikitumiwa na Waarabu kwa nyota mbalimbali na pia kama jina la mwanamume. Suheli inayojulikana zaidi ni Suheli (Alfa Carina) katika kundinyota la Mkuku[2].

Umoja wa Kimataifa wa Astronomia haikuamua bado jina kwa matumizi ya kimataifa; wakati mwingine Gamma Velorum inatajwa kwa tahajia ya “Suhail al Muhlif”, wakati mwingine kwa jina la kisasa “Regor” lililotungwa kwa heshima ya Roger Chaffee, mwanaanga wa NASA aliyekufa katika moto wakati wa kufanya majaribio ya chombo cha angani Apollo 1 kwenye mwaka .

Gamma Velorum ni jina la Bayer. Nyota za Tanga (Vela) zilikuwa sehemu ya kundinyota la kale la Argo na Gamma ilikuwa na mwangaza kwenye nafasi ya tatu. Hapo Nicolas Louis de Lacaille alitoa herufi za Kigiriki kwa nyota za Argo lakini baadaye aligawa Argo katika makundinyota matatu za Shetri (Puppis), Mkuku (Carina) na Tanga (Vela). Baada ya ugawaji huo hakutoa herufi za Kigiriki upya hivyo hakuna Alfa wala Beta katika Tanga.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Suheli katika Tanga ni mfumo wa nyota angalau nne, labda zaidi. Ilitazamwa tangu muda mrefu kuwa nyota maradufu ya nyota mbili za A na B.

Kwa kutumia darubini kubwa zaidi na utafiti wa spektra ilionekana ya kwamba kila moja kati ya hizo mbili ni nyota maradufu tena.

Gamma Velorum A ina sehemu mbili: moja ni nyota jitu kuu buluu na nyingine ni nyota ya Wolf-Rayet ambayo inatarajiwa kuendelea kuwa nova itakayofikia mwisho wake katika mlipuko mkubwa. Nyota hizo mbili ziko kwa umbali wa kizio astronomia kimoja zikizungukana katika muda wa siku 78.5.

Suheli katika Tanga ni nyota ya Wolf-Rayet iliyo karibu na Jua letu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. ling. Knappert 1993
  2. Allen, Star-Names (1899), uk. 72

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 437 (online kwenye archive.org)
  • Roche, P. F.; Colling, M. D.; Barlow, M. J. (2012). "The outer wind of γ Velorum". Monthly Notices of the Royal Astronomical Society. 427: 581 online hapa
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Suheli ya Tanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.