Mwanaanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mfalki Piers Sellers nje ya fasikebu space shuttle tar. 12 Juni 2006

Mfalki au Mwanafasi ni mtu anayezuri fasi nje ya anga ya dunia kusafiria fasikebu ambalo hurushwa angani kwa kutumia fataki.

Mfalki wa kwanza katika historia ya binadamu alikuwa Mrusi Yuri Gagarin kutoka Umoja wa Kisovyeti alipaa tarehe 12 Aprili 1961 kwa fasikebu Vostok akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108.

Alifuatwa 5 Mei 1961 na Alan Shepard kutoka Marekani aliyetumia fasikebu cha Mercury .

Mwanamke wa kwanza kwenye fasi alikuwa Mrusi Valentina Tereshkova mwaka 1963.

Wafalki wa kwanza waliofika kwenye uso wa mwezi walikuwa Wamarekani Neil Armstrong na Buzz Aldrin tar. 20 Julai 1969.

Hadi machi 2008 jumla ya watu 477 kutoka nchi 39 walifika kwenye kimo cha kilomita 100 juu ya uso wa dunia ambacho ni kimo ambako fasi(space) inaanzia kulingana na maelezo ya Shirikisho la Kimataifa la Usafiri wa Fasi (Fédération Aéronautique Internationale (FAI)).

Kati ya hawa ni 24 waliofika mbali zaidi kuliko kilomita 2,000 juu ya uso wa dunia.

Mfalki aliyekaa muda mrefu fasini alikuwa Mrusi Sergei Krikalyov aliyezuru fasi mara sita, akakaa jumla ya siku 803, masaa 9 na dakika 39.

Picha za wafalki tajika

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanaanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.