Alan Shepard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alan Shepard mwezini

Alan Bartlett Shepard, Jr. (18 Novemba 192321 Julai 1998) alikuwa mtu wa pili aliyefika kwenye anga-nje akiwa mwanaanga wa kwanza wa Marekani baada ya Mrusi Yuri Gagarin.

Alijiunga na wanamaji wa jeshi la Marekani akawa rubani na 1959 aliteuliwa kwa mradi wa kuandaa safari kwenda anga-nje. Wakati ule MArekani ilishindana na Umoja wa Kisovieti katika upelelezi wa anga -nje na Marekani ilitarajia kumpeleka mtu wa kwanza angani. Lakini matatizo ya kifundi yalichelewesha safari na Yuri Gagarin aliwatangulia 12 Aprili 1961.

Tarehe 5 Mei 1961 Shepard alirushwa kwa chombo cha Mercury akafikia kimo cha kilomita 187 juu ya uso wa dunia akarudi baada ya dakika 15 na sekunde 22.

Mwaka 1969 aliingizwa katika mradi wa Apollo iliyoandaa safari za kufika mwezini. Alikuwa kiongozi wa safari ya Apollo 14 tar. 31 Januari hadi 9 Februari 1971.

Alibeba kifaa cha golf pamoja na mipira yake akafaulu kupiga mpira wa golf kwenye uso wa mwezi.