Golf
![]() | Unganisha! Imependekezwa makala hii iunganishwe na Gofu (michezo). Ili kupata sababu angalia ukurasa wa majadiliano. |
Golf ni mchezo ambako mchezaji anapiga mpira mdogo kwenye uwanja mkubwa kwa kutumia mafimbo ya pekee akilenga kufikisha mpira katika mashimo yanayofuatana. Sheria ya kimsingi inasema: "Mchezaji anafikisha mpira kutoka chanzo hadi kufikia shimoni kwa pigo moja au mapigo yanayofuatana."
Uwanja[hariri | hariri chanzo]
Uwanja wa golf kwa kawaida ni eneo kubwa inayoweza kufikia hektari 60 hadi 80. Sehemu kubwa ya eneo linafunikwa na manyasi na miti. Uwanja kamili huwa na mashimo 18, uwanja mdogo na mashimo 9.
Kucheza[hariri | hariri chanzo]
Kuanzia chanzo kinachoitwa "tee" mchezaji anaelekea mashimo ya uwanja kwa utaratibu wake; maana anahitaji kufika kwanza shimo na. 1, halafu na. 2 na kadhalika. Lengo ni kufikisha mpira shimoni kwa mapigo machache iwezekanavyo. Idadi ya mapigo inaandikwa na kulinganishwa baadaye kwa kusudi la kumpata mshindi kati ya wachezaji wanaomaliza mashimo yote.
Golf huchezwa na mtu pekee yake kwa mazoezi, na wachezaji wawili kati yao au na timu za wachezaji.
Kulingana na umbali wa shimo na ugumu wa eneo mchezaji ana chaguo kati ya mafimbo mbalimbali. Kwa pigo la mbali atatumia fimbo lenye kichwa kizito kinachorusha mpira hewani kuelekea shimo. Akikaribia atatumia kichwa chepesi zaidi kinachoitwa "putter" na kusukuma mpira juu ya ardhi au manyasi kuelekea shimoni
Mafimbo[hariri | hariri chanzo]
Mchezaji anaruhusiwa kutumia mafimbo hadi 14 tofauti kwa mchezo wake. Wanatofautisha "ubao", "chuma" na "putter".
Mashindano makuu[hariri | hariri chanzo]
Kuna mashindano kadhaa maarufu na hapo hushiriki hasa wachezaji wanaocheza kikazi. Mashindano haya huitwa "majors".
- Wanaume
- The Masters
- U.S. Open
- The Open Championship (British Open)
- PGA Championship
- Wanawake
- Kraft Nabisco Championship
- LPGA Championship
- U.S. Women's Open
- Women's British Open
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
[1] GDO
Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]
- Best Players
- Rules of Golf
- Golf Equipment Reviews
- Golf ball aerodynamics
- Golfers' Dictionary
- A Nice Golf Tips Blog
- Golf news
- Golf history
- Golf trivia
- Golf Tips & More
- Titleist Golf Clubs
- Golf swing tips
- Online Golf Tips & Biomechanics of the golf swing
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Golf kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |