Gofu (michezo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mchezaji gofu Tiger Wooda kutoka Marekani akirusha mpira
Mchezaji gofu akielekea kuzamisha mpira shimoni

Gofu (toka Kiingereza: "golf") ni mchezo ambapo wachezaji wake wanashindana kufikisha mipira midogo kwenye mashimo katika ardhi ya uwanja kwa kuipiga mara chache iwezekanavyo wakitumia fimbo za pekee.

Kwa kawaida uwanja wa gofu huwa na mashimo 18 au 9. Wachezaji wawili au timu mbili huanza mahali pamoja na kupita kwenye mashimo kwa ufuatano uliopangwa.

Shimo linafikiwa kwa kupiga mara moja au mbili kwa nguvu yaani kuvukia umbali mkubwa na baadaye kwa nguvu kidogo ambako ni muhimu kulenga mpira vizuri mpaka inaanguka katika shimo dogo.

Hapa wachezaji huwa na chaguo la aina tofauti za vingoe au "klabu". Kingoe cha gofu kizito kinamwezesha mchezaji kupiga kwa nguvu kubwa na kurusha mpira mbali. Kwa kazi kumu ya kuulenga shimo kina vingoe vyepesi zaidi. Machezaji huchagua seti ya vingoe vyake kabla ya mchezo anaruhusiwa kubeba hadi jumla ya 14 tofauti.

Michezo inayofanana na gofu ilijulikana katika nchi na tamaduni mbalimbali lakini chanzo cha gofu cha kisasa kinaaminiwa kipo Uskoti. Tangu karne ya 18 wachezaji waliungana katika shirika (golf club) na polepole wakaanza kupatana kanuni za mchezo kwa kusudi ya mashindano. Mwaka 1900 na 1904 gofu ilikuwa sehemu ya michezo ya Olimpiki. Mwaka 1971 mwanaanga Alan Shepard alibeba mpira na kingoe hadi mwezi alipopiga mpira huu mara mbili.

Kwa muda mrefu gofu ilikuwa mchezo wa watu wenye pesa kwa sababu kukodi na kutunza kwa uwanja kuna gharama kubwa kiasi. Uwanja wa gofu huwa na hektari 50 au zaidi, yaani kama ekari 120. Kwa mashindano eneo hili linahitaji kutunzwa vema hata kwa mashine za pekee hivyo linahitaji wafanyakazi. Pia vifaa kama mipira na vingoe vilikuwa na gharama kubwa. Siku hizi mchezo umenea zaidi na gharama zimeshuka katika nchi nyingi.

Tovuti za nje[hariri | hariri chanzo]

Football.svg Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gofu (michezo) kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.