Yuri Gagarin
Yuri Alexeyevich Gagarin (Kirusi Юрий Алексеевич Гагарин), alizaliwa tarehe 9 Machi 1934 huko Klushino karibu na Smolensk, Urusi; alifariki tarehe 27 Machi 1968. Alikuwa mwanaanga wa kwanza katika historia yaani mtu wa kwanza aliyefika kwenye [[Anga-nje].
Alimwoa Valentina Goryachova akawa na mabinti wawili ambao ni Galina na Yelena. Akajiunga na Jeshi la Anga ya Urusi mwaka 1955.
Mwaka 1960 aliteuliwa katika kikosi cha kwanza cha marubani walioandaliwa kurushwa kwa anga-nje akateuliwa kuwa mtu wa kwanza wa kutoka duniani.
Tarehe 12 Aprili 1961 alirushwa na chombo cha angani Vostok 1 akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108. Akashuka Siberia.
Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo cha kuandaa wanaanga Warusi. Mwaka 1968 alikufa katika ajali ya ndege alipofanya mazoezi ya urubani akazikwa kwenye makaburi ya heshima huko Moscow.
![]() |
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yuri Gagarin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |